January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walimu waanzisha benki

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba

Spread the love

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kipo kwenye mchakato wa kuazisha Benki ya Biashara ya Wananchi itakayo toa huduma zake nchi nzima. Benki hiyo itaitwa Mwalimu Commecial Banki Plc. Anaandika Sarafina Lidwino… (endelea).

 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Rais wa CWT, Gratian Mukoba, amesema banki hiyo imeshakamilishiwa taratibu zote za usajili katika Mmlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA)  na imeorodheshwa  kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE) kwa ajili ya kuuza hisa kwa waalimu na wananchi wote kwa ujumla.

Mukoba amesema, maombi ya kuuza hisa za banki hiyo yameshakubaliwa na CMSA kwa ajili ya kuaza kuuza hisa hizo.

Amesema, hadi sasa CWT na Kampuni ya Maendeleo ya Walimu Tanzania (TDCL) wamekwishawekeza mtaji wa sh. bilioni 17 katika benki hiyo, na inatarajia kuongeza mtaji wa sh. bilioni 25.

Hata hivyo, Mukoba amesema, uuzaji wa hisa hizo kwa walimu na Watanzania wote kwa ujumla unatarajia kuanza tarehe 23 Machi hadi 4 Mei 2015.

Ameongeza kuwa baada ya uuzaji wa hisa hizo kukamilika katika pindi cha mwezi mmoja, taratibu za kuwasilisha majina ya wanahisa Banki Kuu ya Tanzania (BOT) zitafanyika kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki na kupata leseni.

Benki ya Mwalimu Commecial Plc itamilikiwa kwa pamoja na CWT na Kampuni ya Maendeleo ya Waalimu (TDCL) na wananchi watakao nunua hisa.

Mukoba ametoa wito kwa waalimu wanunue hisa ili kuongeza mtaji wa benki, ambayo inatarajia kufungua shughuli zake rasmi tarehe 2 Novemba 2015.

error: Content is protected !!