July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walimu Sekondari Selina Kombani wamtuhumu Ofisa Elimu

Spread the love

WALIMU kuhamishwa mara kwa mara kutoka Shule ya Sekondari Selina Kombani iliyopo katika Wilaya ya Ulanga kunalenga kuinua kiwango cha taaluma kilichoshuka shuleni hapo, anaandika Christina Raphael.

Kauli hiyo imetolewa na Eprahim Simbeye, Ofisa Elimu wa Mkoa wa Morogoro na kwamba, kumekuwepo malalamiko kutoka kwa wazazi wenye watoto wanaosoma shuleni hapo wakidai kuwa walimu 10 wameshahamishwa bila sababu maalum.

Amesema kuwa, suala la kuhamisha walimu mara kwa mara ni agizo la mkoa lilitokana na walimu wenyewe kuwa na migongano ya mara kwa mara ya walimu na wanafunzi ilisababisha walimu kutoingia darasani kufundisha na hatimaye kushuka kwa kiwango cha taaluma.

Hata hivyo amesema, shule hiyo inakabiliwa na uchache wa walimu hasa wa masomo ya Sayansi na Hisabati ambapo mpaka sasa ina jumla ya wanafunzi 390 huku ikiwa na walimu 18 pekee.

Awali wazazi wa watoto wanaosoma shuleni humo walidai kuwa, wamesikitishwa na kitendo cha ofisa huyo kuhamisha walimu kila kukicha na kufanya ushawishi ili na wengine waache.

error: Content is protected !!