February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Walimu Pemba wapigwa marufuku kwenda harusini

Baadhi ya Walimu wa shule za sekondari na msingi mkoani Pemba

Spread the love

WALIMU wa Shule za msingi na sekondari katika mkoa wa Kaskazini Pemba visiwani Zanzibar wamepigwa marufuku kwenda katika sherehe hasa harusi wakati wa kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Omar Khamis Othman, kwa kusema kuwa serikali haitamvumulia mwalimu atakayetoroka shule kwenda harusini, na kwamba atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria.

RC Othman amesema kuwa, baadhi ya walimu wamekuwa na desturi ya kwenda harusini wakati wa muda wa kazi hasa siku za ijumaa, ambapo amekemea tabia hiyo kwa kuwa ni kinyume na sheria za utumishi wa umma.

Aidha, amewataka wakuu wa shule mkoani humo kutotoa ruhusa kwa walimu wenye tabia za kuondoka shule wakati wa kazi kwa ajili ya kwenda katika sherehe mbalimbali, na kuagiza walimu hao kama wanataka kwenda shughulini kusubiri muda wa kazi utakapoisha.

error: Content is protected !!