August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walimu kujinyakulia ‘tablets’ za sensa

Spread the love

SERIKALI imesema itagawa vishkwambi (tablets) vinavyotumiwa na waratibu wa zoezi la sensa ya watu na makazi nchini kwa walimu wa shule za msingi na sekondari ili kupunguza matumizi ya karatasi katika kutekeleza majukumu yao.

Pia imetenga kiasi cha Sh bilioni moja kwa walimu, wakufunzi au wahadhiri watakaofanya utafiti bora wa kisayansi na elimu tiba na kuchapishwa kwenye majarida maarufu duniani ya Lancet na Nature. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Hayo yamebainishwa leo tarehe 29 Julai, 2022 jijini Dar es Salaam Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kuelezea mwelekeo wa elimu katika mwaka wa fedha 2022/23.

“Mhadhiri yeyote atakayefanya utafiti wa kisayansi na elimu tiba kisha kuchapishwa kwenye majarida ya Lancet na Nature tutampatia zawadi ya Sh milioni 50,” alisema Prof. Mkenda.

Alitolea mfano hospitali ya Kibong’oto iliyopo mkoani Kilimanjaro kwamba watafiti ambao ni watanzania wamefanya utafiti ambao umewezesha kupunguza muda wa matumizi ya dawa za matibabu ya kifua kikuu, hivyo ni vema tafiti za aina hii ziendelee kwa magonjwa mengine kama vile malaria.

ELIMU BURE

Akizungumzia changamoto zilizojitokeza kuhusu utoaji wa elimu bila ada au elimu bure ambayo sasa inatolewa kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita, alisema hivi karibuni Serikali itakuja na muongozo kuhusu mpango huo.

“Nimeongea na Kamisha wa Elimu apitie mwongozo wa michango shuleni michango ni ya hiari na mtoto yeyote asirudishwe nyumbani kwa ajili ya kutotoa michango,” alisema.

Kuhusu mpango wa kuwarejesha shule wanafunzi waliopata ujauzito na kujifungua, Prof Mkenda alisema unaendelea kutekelezwa vizuri nchini.

Aidha, alisema si kweli kwamba mpango huo unahamasisha mimba za utotoni, bali unalenga kumuokoa mtoto wa kike ili apate elimu sawa na watoto wa kiume.

error: Content is protected !!