PATRICK Cheche, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kimataifa Hazina pamoja na walimu wanne wa shule hiyo, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kwa tuhuma za kuvujisha mtihani wa taifa wa darasa la saba. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Washtakiwa hao ambao ni pamoja na Mwalimu Mambo Iddi, Laurence Ochieng, Nasri Mohammed na Justus James walisomewa mashataka leo tarehe 26 Septemba 2018 na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Waalimu hao wanadaiwa kuwapa maudhui ya mtihani wa taifa wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya Hazina.
Baada ya kusomewa mashtaka, watuhumiwa hao walikana mashtaka wanayodaiwa kufanya tarehe 5 Septemba 2018 kwa kuingilia mtihani wa taifa isivyo halali kwa kuwaonyesha watahiniwa maudhui ya mtihani.
Baada ya watuhumiwa kukana mashtaka, kesi hiyo imepangwa kutajwa tarehe 10 Oktoba mwaka huu.
Leave a comment