July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Walimu 106,753 wamepanda vyeo’

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga

Spread the love

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imesema kuwa imekuwa ikitoa miongozo ya kusimamia utoaji wa  mikopo ya elimu ya juu kwa fani mbalimbali ikiwemo ya ualimu. Anaandika Dany Tibason …(endelea).

Akijibu swali la mbunge wa Mufindi Kusini, Mendrad Kigola (CCM) kwa niaba ya wizara hiyo, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, amesema kuwa wanafunzi wote wanaosoma programu hiyo wanapewa mikopo kupitia bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.

Kigola katika swali lake alitaka kujua kama Serikali ipo tayari kutoa mikopo kwa asilimia mia kwa wanafunzi wanaosomea masomo ya ualimu.

Pia alitaka kujua kama serikali haioni umuhimu wa kuongeza ufadhili kwa wanafunzi wanaochukua masomo ya Sayansi ili kupata walimu katika shule za sekondari.

Katika swali hilo pia, Kigola alihoji kama serikali haioni haja ya kupandisha vyeo au madaraja walimu waliojiendeleza kimasomo badala ya kuwaacha na madaraja ya chini na kuwakatisha tamaa ya kujiendeleza.

Akijibu maswali hayo, Dk. Mahanga amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano yaani Juni 2010 hadi Aprili 2015, serikali iliwapandisha vyeo/madaraja walimu 106,753 wa shule ya msingi na sekondari katika ngazi mbalimbali.

Amesema katika juhudi za serikali za kupunguza uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi na hisabati kuanzia mwaka 2014 hadi mwaka huu, serikali ilianzisha program maalum ya Diplopma ya Sayansi na hisabati katika Chuo Kikuu cha Dodoma.

Kwa mujibu wa Dk. Mahanga, ilianzishwa diploma ya juu ya Ualimu wa Sayansi na Hisababti katika vyuo vikuu vya ualimu vya Korogwe, Kleruu na Monduli.

error: Content is protected !!