Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Walevi wa ngono kukiona  
Habari za Siasa

Walevi wa ngono kukiona  

Spread the love

WATU wanaopenda kufanya ngono na wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari nchini sasa kukamatwa. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kazi ya kuanza kukabiliana na watu wenye tabia hiyo inaanzia mkoani Kilimanjaro ambapo Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu ameagiza waliowapa mimba wanafunzi mkoani humo wakamatwe.

Ni baada ya taarifa ya mkoa huo kuonesha kwamba, kuanzia Januari hadi Desemba mwaka 2018, jumla ya wanafunzi wa kike 57 walipachikwa mimba na hatimaye kukatisha masomo yao.

Taarifa hiyo ilimshtua Waziri Majaliwa na hasa baada ya kuelezwa kuwa, katika kesi hizo 57 za wanafunzi kupachikwa mimba, ni kesi sita tu ndio zilizofikishwa mahakamani.

Agizo hilo la kukamatwa malevi hao wa ngono wote limetolewa na Waziri Majaliwa mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano uliofanyika katika Uwanja wa Isanja, Sanya Juu katika Wilaya ya Siha, Kilimanjaro.

Wakati Waziri Majaliwa akitoa onyo hilo, Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imeeleza kuwa, Virusi Vinavyosababisha Ukimwi (VVU) vinaendelea kusambaa na kwamba, wananchi wanapaswa kuwa na tahadhari.

Takwimu zilizotolewa na Juma Billingi, Kamshna wa TACAIDS Mkoa wa Tanga tarehe 24 Julai 2018 wilayani Bagamoyo, Pwani katika utafitiwa uliofanyika mwaka 2016/17 unaonesha kuwa, Mkoa wa Kilimanjaro una asilimi 3.8 ya maambukizi ya VVU.

Waziri Majaliwa alitoa kauli ya kukamatwa kwa watu wao kwenye mkutano wa mwisho katika ziara yake aliyoifanya mkoani humo ambapo alisema, tabia ya watu hao haivumiliki huku akihoji, inakuwaje kesi hizo hazifikishwi mahakamani.

Waziri Majaliwa amesema, serikali imeweka sheria kali kwa ajili ya kuhakikisha mtoto wa kike analindwa ili kutimiza malengo ikiwa ni pamoja na kuhitimu masomo yake.

Amesema, miongoni mwa adhabu hizo ni kifungo cha miaka 30 kwa yule atakayebainika kutenda kosa hilo kwa mujibu wa sheria.

“Haiwezekani. Hakikisheni waliohusika wote kuwapa mimba wanafunzi hawa wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria,” amesema Waziri Majaliwa na kuongeza;

“Ole wenu vijana, siku mkibainika kuwapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela, sasa tafakari kabla ya kutenda.”

Hata hivyo, Waziri Majaliwa ameonya tabia ya wazazi wa watoto waliopewa mimba kwamba, wamekuwa wakikutana na wahusika na kisha kumalizana kwa kupewa ngo’ombe ama kitu chochote.

“Kuanzaia sasa tukikukata unamalizana na mtu aliyempa mimba mwanafunzi na wewe tunakufunga,” amesema.

Idadi ya wanafunzi waliokatisha masomo kwa sababu ya mimba katika shule za msingi na sekondari nchini, imeongezeka kutoka takribani 3,000 ya mwaka 2013 hadi wanafunzi 5,033 katika mwaka 2016.

takwimu hizo zilitolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Watoto katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Margaret Mussai wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita mimba za utotoni na rushwa mkoani Dodoma mwaka jana.

Alisema pia baadhi ya wanafunzi wanapata mimba kutokana na ukatili unaofanywa nyumbani na ndugu, jamaa na marafiki unaofikia takriban asilimia 60, huku asilimia 40 zinazobaki, watoto wakifanyiwa ukatili shuleni na baadhi ya walimu na viongozi wengine.

Ifuatayo ni orodha ya maambukizi ya VVU kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na TACAIDS 216/17;-

Njombe asilimia 14.8, Iringa asilimia 9.1, Mbeya asilimia 9.0, Shinyanga asilimia 7.4 Ruvuma asilimia 7.0 Dar es Salaam asilimia 6.9, Rukwa asilimia 6.2, Katavi asilimia 5.9.

Pia Pwani asilimia 5.9 Tabora asilimia 5.1,Kagera asilimia 4.8, Geita asilimia 4.7 Mara asilimia 4.5, Mtwara asilimia, Morogoro asilimia 3.8, Shinyanga asilimia 3.6.

Manyara asilimia 3.2, Singida 3.3, Tanga asilimia 2.4, Dodoma, asilimia 2.9 na Lindi asilimia 2.9 , Kaskazini Pemba 0.3, Kusini Pemba asilimia 0.4 , Kaskaziniu Unguja asilimia 0.1 kusini Unguja asilimia 0.5 na Mjini Magharibi asilimia 1.4.

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

error: Content is protected !!