January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walemavu waitaka NEC iwajali

Spread the love

WATU wenye ulemavu nchini wameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuangalia uwezekani wa kuangalia changamoto zinazowakabili kulingana na mahitaji ya kila kundi ili kuwatengenezea mazingira mazuri ya kupiga kura kwenye uchaguzi ujao Oktoba 25 mwaka huu. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Wakizungumza na waandishi leo Jijini Dar es Salaam, walemavu hao kutoka makundi mbalimbali wamesema, kila kundi lina mahitaji yake kutokana na ulemavu wake.

Meneja Miradi wa (CCBRT), Fredrick Muigallah amesema kuwa elimu ya kwa wapiga kura walemavu kutokana na elimu hiyo inawafikia watu wanaoishi mjini.

Pia alieleza jinsi gani msimamizi wa kituo cha kupiga kura atabaini kuwa mpigaji kura kuwa ni kiziwi au ana ulemavu usionekana.

Katibu Mkuu wa Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu(SWAUTA), Stella Jailos ambaye ni mlemavu wa macho amesema kuwa utaratibu wa mtu wa kusindikizwa katika kupiga kura sio mzuri ambapo anawapongeza (NEC) kwa kuandaa karatasi za kupiga kura zenye nukta nundu.

Katibu mkuu wa Shirikisho la Vyama vya watu Ulemavu Tanzania(SHIVAWATA), Felician Mkude amesema kuwa vyama vya siasa havijaanda mazingira mazuri ya usalama katika kampeni zao .Pia kutengeneza ilani zinazogusa maslahi ya walemavu.

error: Content is protected !!