Tuesday , 30 May 2023
Home Habari Mchanganyiko Walemavu Dodoma kuendelea kubaki masikini
Habari Mchanganyiko

Walemavu Dodoma kuendelea kubaki masikini

Spread the love

CHANGAMOTO ya vikundi vya watu wenye ulemavu katika mkoa wa Dodoma kushindwa kuchangamkia fursa ya kupata fedha za mikopo zinazitolewa na halmashauri katika mkoa huo, inaweza kuwa sababisho la vikundi hivyo kuendelea kuwa masikini. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Hali hiyo inatajwa kuwa ni kutokana na vikundi hivyo vilivyo kushindwa kutojitokeza licha ya kuwa ni vikundi vingi lakini kati ya vikundi hivyo ni vikundi vinne vya halmashauri ya Jiji la Dodoma ndivyo wamechukua mkopo huku halmashauri nyingine saba hakuna kikundi hata kimoja kilichojitokeza kuomba mkopo.

Hayo yalibainishwa kweye hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge wakati wa maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu ambayo ilisomwa kwa niaba yake na mkuu wa wilaya ya Chemba, Simon Odunga.

Odunga kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma alisema asilimia mbili ya mapato ya halmashauri hutengwa kwa ajili ya kukopesha watu wenye ulemavu na kuvitaka vikundi kujitokeza ili kuchukua mikopo hiyo na kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Alisema hata hivyo pamoja na kutengwa huko kwa asilimia hizo ni vikundi kutoka jiji ndivyo vimechangamikia fursa hiyo huku halmashauri nyingine saba hakuna kikundi hata kimoja kilichochukua mkopo .

Pia aliagiza wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Dodoma wametakiwa kuhakikisha wanakamilisha zoezi la utambuzi la watu wenye ulemavu ifikapo Machi mwakani ili kujumuishwa kwenye mpango wa serikali.

Aidha wakuu hao wa wilaya wameagizwa kuhakikisha wanatenga maeneo ya kufanyia biashara watu wenye ulemavu na taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo liwasilishwe Ofisi ya mkoa ifikapo Machi 30, mwakani.

Alisema kumekuwa na changamoto ya kuwa na takwimu ambazo si sahihi lakini sasa inatakiwa kuwatambua watu wote wenye ulemavu na mahali walipo

Odunga alisema katika sense ya watu na makazi ya mwaka 2012 ilionesha kuwa mkoa wa Dodoma ulikuwa na jumla ya watu wapatao 2,083,588 kati ya hao watu wenye ulemavu walikuwa 106,414.

Alisema kulingana na takwimu hizo walemavu wa ngozi (albino) walikuwa 1,034 waliotambuliwa walikuwa 280, wasioona 41,985 waliotambuliwa 9,916, viziwi, 22,512 waliotambulia 2,017, walemavu wa viungo 23,124 waliotambuliwa 13,063, walemavu wa akili 17,759 waliotambuliwa 2,232 ambapo jumla ya walemavu waliotambuliwa walikuwa ni 27,598.

‘’Bado utambuzi unaendelea ingawa si wa kiwango cha kuridhisha, nawaagiza wakuu wa wilaya zote kuhakikisha wanakamilisha zoezi la utambuzi wa watu wenye ulemavu ifikapo Machi mwakani,” alisema Odunga.

Pia aliwataka watu wenye ulemavu kushiriki vyema katika kamati za watu wenye ulemavu kwani ni agizo la kisheria na lazima litekelezwe.

Alisema bado kuna changamoto ya ukosefu wa ajira kwa watu wenye ulemavu aliwataka waajiri katika halmashauri za mkoa kuzingatia sheria namba tisa ya mwaka 2010 inayowaagiza wenye utumishi kuanzia 20 na kuendelea kutenga asilimia tatu ya ajira za watu wenye ulemavu.

Naye Meneja wa Mradi wa Elimu Jumuishi kutoka Tanzania Cheshire Foundation (TCF), Ledman Mjema alisema mradi unakusudia kuandikisha  watoto 1,000 katika shule za msingi 20 ambapo mpaka sasa mradi unahudumia watoto 380 walioko mashuleni.

Alisema mpaka sasa mradi wake wa elimu jumuishi unaoendelezwa katika wilaya ya Dodoma na Chamwino na umefanikiwa kuwatambua wanafunzi kiafya na uwezo wa kielimu kwa  kuwafikia mashuleni zaidi ya watoto 16,000.

Alisema watoto hao ambao wenye ulemavu wamefanikiwa kuwezeshwa vifaa mbalimbali vikiwemo sare za shule, vifaa vya kujifunzia, vifaa visaidizi kama baiskeli ya magurudumu matatu na miwani ya kusomea na bado zoezi hilo linaendelea.

Kwa upande wake Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu, Jastus Ng’antalima alisema kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inalenga kuwawezesha na kuwajumuisha watu wenye ulemavu ili waweze kushiriki masuala mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa usawa ifikapo mwaka 2030.

Awali akizungumza kwenye maadhimisho hayo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alitaka wananchi kusaidia watu wenye ulemavu katika maeneo mbalimbali bila kuwabagua kutokana na hali zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wenye ulemavu waiomba MISA-TAN iwajengee uwezo wa uhuru wa kujieleza

Spread the love  TAASISI ya vyombo vya Habari kusini mwa Afrika (MISA-TAN)...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wajawazito 2000 Korogwe washiriki Marathon, Mwenyekiti UWT amsifu Jokate

Spread the loveWANAWAKE wajawazito zaidi ya 2000 wilayani Korogwe mkoani Tanga wameshiriki...

Habari Mchanganyiko

Kirigini kuzikwa leo Butiama

Spread the love  MWILI wa aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini (1980-1985), Herman...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

error: Content is protected !!