July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Walaji fedha za TASAF matatani

Spread the love

TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Morogoro imewaasa viongozi wa Serikali wanaodaiwa kufuja fedha zinazotolewa na mfuko wa kusaidia kaya maskini (TASAF) huku walengwa wakiachwa bila msaada wowote, anaandika Christina Raphael, Morogoro.

Emmanuel Kiyabo, Kamanda wa TAKUKURU mkoani Morogoro, alitoa rai hiyo jana wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema wameanzisha uchunguzi katika wilaya ya Mvomero na Gairo na tayari wameshabaini baadhi ya viongozi kutafuna fedha hizo.

Aidha Kiyabo amesema kuwa taasisi hiyo haitasita kuwachukulia hatua kali viongozi watakaohusika na ulaji wa fedha hizo huku wakienda kinyume na malengo ya serikali kuwasaidia wananchi kupambana umasikini.

“Tumegundua kuna viongozi wanakula fedha za kaya maskini, na hazifiki kwa walengwa hali iliyotusukuma kuanza uchunguzi ili kukomesha tabia hiyo,” amesema Kiyabo.

Hivyo aliwataka viongozi wanaohusika na wizi na ubadhilifu huo kuacha mara moja kabla mkono wa sheria haujawafikia na adhabu kali kutolewa dhidi yao.

Hata hivyo Kiyabo aliwataka wananchi wote wanaojua walistahili kupata fedha hizo lakini kwa sababu zisizoeleweka hawakuweza kupata wafike ofisini za TAKUKURU mkoa ili wapate msaada.

Kamanda huyo amesema kuwa kimsingi fedha hizo zinatakiwa kuwafikia walengwa kwa asilimia 100 na kwamba kwa sasa suala hilo limekuwa halitekelezwi kikamilifu.

error: Content is protected !!