January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakuu wa vyuo vya kodi kukutana Tanzania

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Spread the love

TANZANIA imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa wakuu wa vyuo vya uongozi wa kodi barani Afrika, pamoja na wakuu wa mafunzo katika taasisi za kodi. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Mkutano huo utafanyika kwa siku tatu, kuanzia tarehe 27-29 katika ukumbi wa hotel ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mkutano huo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo, amesema, “niheshima kubwa kwa Tanzania kuchaguliwa kuwa  mwenyeji wa mkutano huu wa kwanza, ambapo tunakutana kujadili masuala muhimu ya kujenga uwezo”.

Amesema, mkutano utakuwa chini ya usimamizi wa TRA, kupitia uongozi wa chuo cha kodi (ITA) pamoja na Taasisi za kodi Afrika (Africa Tax Administration Forum, ATAF utajumisha zaidi ya wajumbe 50 kutoka vyuo vya kodi barani Afrika.

Lengo la mkutano huo ni kuweza kujadili hatua iliyofikiwa na ATAF kwenye programu yake ya kujenga uwezo na kuendeleza rasilimali watu kwenye uongozi na usimamizi wa kodi barani Afrika.

Kayombo amesema, katika mkutano huo wajumbe watapata fursa ya kujadili hatua iliyofikiwa mpaka sasa katika jitihada za pamoja za kujenga uwezo baina ya nchi za Afrika katika suala zima la uongozi na usimamizi wa kodi na kuwa na mtandao wa kujenga ushirikiano ambao utanufaisha nchi zote.

“ATAF ilitengeneza mkakati wa kujenga uwezo mwaka 2014, na inasisitiza umuhimu wa nchi zote wanachama kushiriki katika utekelezaji wa mkakati huu. Na unakusudia kuanzisha chuo cha Afrika cha uongozi wa kodi na kuwa na kituo maalumu cha kutoa msaada wa kiufundi kwenye masuala ya kodi.” amesema Kayombo.

Aidha, lengo lingine la ATAF ni kuwa na jukwaa ambalo wasimamizi wa kodi barani Afrika wanaweza kushirikiana kwa pamoja, kubadilishana mawazo, uzoefu ili kuboresha ukusanyaji wa kodi. Pia inalenga kusaidia nchi wanachama 54 ziweze kushirikiana, kuwa na sera moja.

Ameeleza kuwa baadhi ya nchi wanachama wa ATAF ni pamoja na Benin, Botswana, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Chad, Gabon, Ghana, Kenya, Lesotho, Nigeria, Sudani, Rwanda, Uganda, Sierra Leone, Swazland, Senegal, Ghambia, Tanzania, Zimbabwe, Malawi na Namibia.

error: Content is protected !!