Spread the love

 

OMBI la nchi ya Kidemokrasia ya Congo ( DRC), kujiunga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), linatarajiwa kujadiliwa tarehe 22 Desemba 2021. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea)

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumamosi, tarehe 18 desemba 2021 na Afisa Mahusiano Mwandamizi wa EAC, Simon Peter Owaka, akitoa ratiba ya mkutano wa wakuu wa nchi mwanachama wa jumuiya hiyo, unaotarajiwa kufanyika kwa njia ya mtandao.

Mbali na kujadili ombi hilo, taarifa ya Owaka imesema wakuu hao wa nchi, watajadili marekebisho ya kanuni ya akidi ya mkutano wa EAC.

“Wakuu wa nchi za EAC wamepangwa kuitisha mkutano wa 18, unaotarajiwa kufanyika kwa njia ya mtandao, Jumatano tarehe 22 Desemba 2021, mkutano huo unatarajia kujadili mambo mawili, ripoti ya Baraza la Mawaziri juu ya uandikishaji wa DRC na marekebisho ya akidi ya mkutano,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa ya Owaka imesema kuwa, mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa 45 wa Baraza la Mawaziri wa EAC, utakaofanyika tarehe 20 Desemba 2021.

Juni 2019, akiwa katika ziara yake ya kikazi nchini Tanzania, Rais wa DRC, Felix Tshisekedi, alisema nchi yake imeomba kujiunga na EAC, kwa kuwa ni jumuiya muhimu duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *