July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakuu wa mashirika, bodi kufanyiwa usaili badala ya teuzi

Waziri wa Fedha na Mpango wa Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba

Spread the love

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amependekeza wakuu wa mashirika kupatikana kwa ushindani kwa kufanyiwa usaili ili kupata watu wenye sifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea)

Amependekeza pia utaratibu huohuo utumike kwa wajumbe wa bodi za mashirika ya umma.
Dk. Nchemba, ameyasema hayo leo Jumanne tarehe 14 Juni, 2022 akiwasilisha bungeni bajeti kuu ya Serikali.

Dk. Mwigulu amesema anapendekeza nafasi zianze kutangazwa pale nafasi inapokuwa wazi.
“Wenye sifa ndio wafanyiwe upekuzi kufanyiwa uteuzi na kupewa mkataba wenye malengo yanayopimika,” amesema.

“Mashirika na taasisi zingine, bodi na Menejimenti zimezidisha urafiki sana na wanaendesha ofisi kirafiki, hakuna uwajibikaji wa kutosha, hii inakiuka misingi ya mashirika kuwa na bodi za wakurugenzi.

Hii inasababisha watu wakikabidhiwa shirika la umma wanageuza ni mali yao au duka,” ameongeza.

Aidha amependekeza mashirika yote ya umma yenye kufanya kazi kwa misingi ya kibiashara yafanye kazi kwa ufanisi na faida.

Amesema kwa yale yasiyofanya kazi kibiashara watayapima kwa namna wanavyowezesha uchumi kuchangamka na jinsi wanavyoimarisha huduma wanazozitoa kwa jamii.

“Mashirika mengi ni mzigo kwa Serikali kwa kutegemea ruzuku kutoka serikalini ili yajiendeshe,” amesema na kueleza zaidi kuwa kwa nchi zilizoendelea, mapato makubwa ya Serikali yanatoka kwenye mashirika yake ili kuwapunguzia mzigo maskini wa kulipa kodi ili ziendeshe mashirika hayo lakini pia kupunguzia Serikali kutegemea kukusanya fedha kutoka kwa watu maskini.

error: Content is protected !!