Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wakurugenzi wa halmashauri tano wakalia kuti kavu
Habari za Siasa

Wakurugenzi wa halmashauri tano wakalia kuti kavu

Suleiman Jafo, Waziri wa Tamisemi
Spread the love

WAKURUGENZI ambao halimashauri zao zimekusanya mapato chini ya asilimia 50, wametakiwa kujitathimini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Halmashauri tano za mwisho kwa makusanyo katika kigezo cha asilimia ni Halmashauri ya Wilaya ya Newala (asilimia 15), Tandahimba (asilimia 15), Momba (asilimia 13), Masasi (asilimia 13) na Nanyamba (asilimia 12). 

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 26 Aprili 2019 na Seleman Jafo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawazala za Mikoa na Serkali za Mitaa mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma.

Jafo amesema hayo wakati akitoa taarifa ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa kipindi cha robo ya tatu (Julai – Machi 2019), kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Amesema, kila halmashauri ijitathmini kwani, taarifa hiyo ni kigezo muhimu kwa kazi nautendeaji wa wakurugenzi wa halmashauri.

“Kila mkurugenzi ataenda kupimwa kwa kazi zake alizozifanya ili kuweza kuthamini kazi zao,” amesema na kuongeza;

“Kuna halmashauri zingine hazitumii mfumo kielektoniki, na badala yake wanatumia mifumo ya kizamani hali ambayo inasababisha kutokuwa na ripoti nzuri za mapato.”

Ametaja halmashauri tano zilizoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani, yaliyokusanywa ukilinganisha na makisio ya halmashauri ya mwaka.

Halmashauri hizo ni Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi ikiongoza kwa asilimia 113, Halmashauri ya Wilaya ya Geita asilimia 109, Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe asilimia 105, Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo asilimia 103 na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga asilimia 92.

Aidha ametaja halmashauri zilizoongoza kwa kigezo cha pato ghafi (wingi wa mapato) yaliyokusanywa ukilinganisha na makisio ya halmashauri ya mwaka.

Nazo ni Halmashauri ya Jiji la Dodoma ikiongoza kwa Sh. 49.9 Bil ikifuatiwa na Ilala Sh. 44.8 Bil, Kinondoni Sh. 23.5 Bil, Temeke Sh. 20.6 Bil na Jiji la Arusha kwa Sh. 12.5 Bil.

Wakati huohuo ametaja halmashauri tano za mwisho kwa kigezo cha pato ghafi (wingi wa mapato) yaliyokusanywa ukilinganisha na makisio ya halmashauri ya mwaka.

Halmashauri hizo ni ya Wilaya ya Madaba, Sh. 293.7 milioni, Newala Sh. 268.3 milioni, Kakonko Sh. 238.6 milioni, Buhigwe Sh. 177.3 milioni na Halmashauri ya Wilaya ya Mombi Sh. 170.4 milioni.

Ametaja mikoa iliyoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani, yaliyokusanywa ukilinganisha na jumla ya makisio ya halmashauri katika mkoa kuwa ni Iringa (asilimia 77), Geita(asilimia 73), Dar es salaam(asilimia 72), Dodoma(asilimia 68)  na Songwe (asilimia 68).

Mikoa ilizoongoza kwa kigezo cha pato ghafi (wingi wa mapato) ni Dar es Saalam Sh. 118.4 Bil, Dodoma Sh. 57.3 Bil, Mwanza Sh. 22.9 Bil, Arusha 22.8 Bil na Mbeya Sh. 19.8 Bil.

Aidha aliitaja mikoa ya mwisho kwa kigezo cha pato ghafi kuwa ni Manyara bilion 6.5, Lindi 6.1, Rukwa 5.8, Kigoma 4.5,na mkoa wa Katavi 3.8.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

error: Content is protected !!