Friday , 9 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Wakurugenzi Halmashauri wachimbwa mkwara
Habari Mchanganyiko

Wakurugenzi Halmashauri wachimbwa mkwara

Waziri wa Muungano, Suleiman Jafo
Spread the love

SERIKALI imesema itamchukulia hatua kali mkurugenzi yoyote wa halmashauri nchini ambaye atashindwa kutenga asilimia kumi ya mapato kwa ajili ya akina mama na vijana. Anaripoti Dany Tibason … (endelea).

Mbali na kushindwa kutenga fedha hiyo pia wakurugenzi watakaoonekana kutenga fedha hizo lakini wakizumia kinyume na sheria ya matumizi ya asilimia kumi kwa ajili ya akina mama na vijana hawatafumbiwa macho watashughulikiwa kikamilifu.

Kauli hiyo ilitolewa leo bungeni na Waziri wa Nchi Ofisi ra Rais –TAMISEMI, Selemani  Jafo alipokuwa akijibu maswali ya nyongeza ya wabunge jana bungeni kutokana na wabunge kutaka kujua ni kwanini serikai halmashauri nyingi hazitekelezi sheria ya makusanyo ya mapato ya halmashauri kwa kutenga asilimia kumi kwa ajili ya vijana na akina mama.

Jafo amesema kuwa serikali haitamfumbia macho mkurugenzi yoyote ambaye atashindwa kutenga asilimia kumi ya mapato ya halmashauri kwa ajili ya akina mama na vijana ambayo utengwa kwa ajili ya maendeleo yao.

Mbali na hilo amesema siyo kushindwa kutenga tu bali pesa hiyo inatakiwa kutengwa na kuwafikia walengwa kwani jambo hilo siyo hihari bali lipo kisheria na zinatakiwa kutolewa kwa vijana na akina mama.

“Nataka kusema kuwa hilo jambo halina mjadala hata kama halmashauri itakuwa imekusanya kiasi cha Sh. 10 lakini ni lazima asilimia kumi itengwe na nataka kuwahakikishia wabunge wote halmashauri ambayo itashindwa kutenga fedha hiyo mkurugenzi ataonewa aibu kabisa na siyo tu kutenga fedha lakini pia zinatakiwa kuwafikia akina mama na vijana kwa mujibu wa sheria,” amesema Jafo.

Awali katika swali la msingi la Mbunge wa Buhigwe, Albert Obama Ntabaliba (CCM) ametaka kujua ni lini serikali itawasaidia kimahitaji vijana na akina mama ili waweze kujikomboa.

Pia mbunge huyo alitaka kujua ni kiasi gani kimetolewa kuwawezesha akina mama na vijana katika mwaka 2010 hadi 2017.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Josephat Kandege, amesema halmashauri ya Buhigwe ilianza kufanya kazi Januari 2013 hivyo taarifa zilizopo ni kuanzia mwaka huo.

Kandege amesema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2013/14 hadi 2016/17 halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe ilitoa jumla ya sh. 25,377,057 kwa ajili ya kuvikopesha vikundi vya wanawake na vijana.

Amesema kwa mwaka wa fedha 2017/18 hadi kufikia Mei jumla ya Sh.10,500,000 zimetolewa katika vikundi vya wanawake na vijana aidha kupitia mfuko wa jimbo mbunge alitoa Sh. 10,500,000 kwa vikundi saba vya bodaboda na kikundi kimoja cha mafundi  seremala.

Kandege amesema jumla ya Sh. 20,200,000 zimetengwa kwa mwaka wa fedha 2018/19 kwa ajili ya vikundi vya wanawake na vijana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!