July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakurugenzi halmashauri kukatwa mishahara

Naibu Waziri wa Kaitba na Sheria, Ummy Mwalimu

Spread the love

SERIKALI imesema kuwa, mkurugenzi yeyote wa halmashauri ambaye hatatenga asilimia tano ya maendeleo ya wanawake atakatwa katika mshahara wake. Anaandika Dany Tibason …. (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Kaitba na Sheria, Ummy Mwalimu alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Omar Juma (CUF) kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

“Serikali imeamua kuwabana wakurugenzi wote wa halmashauri kuhakikisha wanatenga asilimia tano kwa ajili ya maendeleo ya wanawake na mkurugenzi yeyote ambaye hatatenga fedha hizo, atapewa adhabu ya kukatwa katika mshahara wake” alisema Mwalimu.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo aliyetaka kujua serikali ina makakati gani wa kuhakikisha fedha Sh. Bil 2 zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ya kuinua uchumi kwa wanawake inapatikana.

Mbunge huyo alitaka kujua hadi sasa ni mikoa mingapi imefaidika na mfuko huo.

“Katika mwaka wa fedha 2012/2014 serikali ilitenga Sh. Bil 2 kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake katika kipindi cha Julai- Desemba 2013 na wizara ilipokea kiasi cha Sh. Mil 515.6 tu kutoka wizarani.

“Je, serikali ina mkakati gani ya kuhakikisha kuwa fedha hiyo inapatikana ili kuendeleza wanawake kiuchumi. Je, ni mikoa mingapi hadi sasa imefaidika na mfuko huo?” alihoji Riziki.

Akijibu maswali hayo Mwalimu amesema, anakubaliana na mbunge kuwa kwa mwaka wa fedha 2013/14 serikali ilitenga kiasi cha Sh. Bil 2 kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake na katika kipindi cha Julai –Desemba 2013 wizara kutoka hazina ilipokea kiasi cha Sh. Mil 515.6 tu.

Alisema mkakati wa serikali ni kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake ambapo kwa mwaka 2015/16 kiasi cha sh.bilioni 1.5 kimetengwa.

Amesema mikoa yote 25 ya Tanzania Bara imenufaika na fedha za mfuko huo na kwamba, halmashauri zilizopewa fedha hizo zilipewa kutokana na ukubwa wa halmashauri husika.

error: Content is protected !!