Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakuliwa watakiwa kupewa elimu sahihi ya matumizi ya mbolea
Habari Mchanganyiko

Wakuliwa watakiwa kupewa elimu sahihi ya matumizi ya mbolea

Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba
Spread the love

NAIBU Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba amewataka wadau mbalimbali wa maendeleo, maafisa ugani na watafiti kuendelea kujipanga kimkakati kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea na pembejeo zingine ili kuwafanya wakulima kutoogopa matumizi ya mbolea kwa madai ya kuua ardhi zao. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Naibu Waziri huyo aliyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya mbolea duniani yaliyofanyika kitaifa kwenye viwanja vya Ushirika wa Wakulima wadogowadogo wa Kilimo cha Umwagiliaji mpunga Dakawa Limited (UWAWAKUDA) uliopo eneo la Dakawa wilayani Mvomero mkoani hapa ambapo alisema ikiwa wakulima watatumia elimu watayopewa na wataalamu wa kilimo waliopo sambamba na matokeo ya tafiti wanayotoa wataweza kuzalisha kwa tija

Mgumba alisema mbolea inapotumiwa kwa usahihi sambamba na kuzingatia kanuni za kilimo bora ni dhahiri kutakuwa na uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na mkulima kupata malighafi za kutosha kwa ajili ya viwanda.

Alisema serikali imeweka maafisa ugani wa vijiji ili waweze kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi ya teknolojia mbalimbali za kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija sambamba na kuweka vituo vya utafiti wa kilimo katika kila kanda ambavyo wakulima wanapaswa kuvitumia.

Hata hivyo aliwaomba wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye ujenzi wa viwanda vya kutengeneza mbolea nchini ili kuchangia katika ongezeko la upatikanaji wa mbolea na kupunguza bei kwa wakulima.

Loata Ole Sanare, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro

Alisema kuwekeza viwanda kutasaidia upatikanaji wa mbolea nyingi nchini hivyo kuuzwa kwa bei nafuu kwa ajili ya mkulima.

Alisema kuanzishwa kwa viwanda vya kutengeneza mbolea pia kutasaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa ajira kwa vijana na hivyo kuongeza tija na maendeleo ya nchini.

Alisem serikali imejizatiti katika kupitia sera bora na mazingira bora ya uwekezaji kwenye kuongeza uzalishaji wa ndani wa mbolea na visaidizi vyake ambapo katika awamu ya tano ya uongozi wa Rais John Magufuli kulikuwa na viwanda vinne vya mbolea na mpaka sasa kuna jumla ya viwanda nane ambavyo vinazalisha zaidi ya tani 30,000 za mbolea ambazo ni sawa na asilimia 46% ya mahitaji ambayo katika msimu wa mwaka 2019/20 yalikuwa tani 586,604.

Alisema serikali imepata mafanikio makubwa baada ya kumwezesha mkulima mdogo kuwa mwingizaji wa mbolea nchini kupitia mfumo wa uingizwaji na mbolea kwa pamoja (BPS) na kufanya mbolea kumfikia mkulima hadi kijijini katika hali ya ubora kwa wakati na kwa gharama nafuu.

Aidha aliviagiza vyama vya ushirika kuiga mfano wa vyama vingine vilivyoweza kuingiza mbolea baada ya kufuata utaratibu kuanza michakato ya kuingiza mbolea kupitia mfumo wa (BPS).

“Kama wizara yangu ilivyoutangazia umma wakati inatangazwa bei elekezi ya mbolea Agosti 11, 2020, katika zabuni za BPS zilizofunguliwa mwezi Juni 2020 vyama viwili viliagiza mbolea ambazo zilipelekwa moja kwa moja kwa wakulima vijijini ili kusubiri kuanza kwa msimu wa kilimo,” alisema.

Naye Katibu Mkuu wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya alisema wizara itaendelea kusimamia taasisi zake zote zilizopo kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo iliwemo Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) ili kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo bora kwa wakati na kwa bei nafuu.

Alisema wizara pia itasimamia mazao ya wakulima kwa kuhakikisha yanapata soko lenye bei nzuri kwa kuimarisha mifumo husika kupitia hatua za sera ya kilimo ya mwaka 2013 na kutunga sheria ya kilimo ili kuiwezesha sekta ya kilimo kuongeza tija na kujitosheleza kwa chakula, malighafi, za viwandani na kuongeza mchango wake kwenye pato la Taifa.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi TFRA Prof. Anthony Mshandete alisema licha ya kuwa matumizi ya mbolea yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka lakini matumizi hayo bado yapo chini ikilinganishwa na Azimio la Maputo la mwaka 2003 na Azimio la Abuja la mwaka 2006 ambayo yalielekeza kuongezeka kwa matumizi ya mbolea hadi kufikia kilo 50 za virutubisho kwa hekta moja.

Prof. Mshandete alisema matumizi ya mbolea kwa hapa nchini yanakadiriwa kuwa ni kati ya kilo 23-25 za virutubisho kwa hekta moja na kwamba matumizi hayo madogo ya mbolea yamechangiwa na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa elimu juu ya umuhimu wa matumizi sahihi na faida za mbolea na bei kubwa ya mbolea itokanayo na mbolea nyingi kuagizwa nje ya nchi.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mbolea duniani mwaka 2020 ni ‘kuwawezesha wakulima wadogo kupata mbolea bora kwa wakati na kwa bei nafuu.’

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yakabidhi Kombe la Ubingwa wa  Ligi Kuu ya NBC, yaahidi maboresha zaidi

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC (NBC Premiere League),...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

Habari Mchanganyiko

Wanne wadakwa kwa kusafirisha punda 46 nje ya nchi

Spread the loveJeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa...

error: Content is protected !!