January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakulima watakiwa kuwa makini na pembejeo

Spread the love

SERIKALI imewataka wakulima kuwa makini na ubora wa mbolea za mazao yao na kuhakikisha wanatumia ruzuku za pembejeo kwa kutumia vocha kwa lengo husika kuhakikisha wanafikisha ubora mzuri wa mazao kimataifa. Anaandika Hamisi Mguta … (endelea).

Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Richard Kasuga wakati wa kutoa taarifa ya utekelezaji wa ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa njia ya vocha kwa msimu wa kilimo mwaka 2015-16.

Kasuga amesema ili kufanikisha mapinduzi kijani, kwa kutumia pembejeo kwa mfumo wa vocha ni lazima wakulima watambue kuwa wanapoteuliwa kwa kupewa vocha wanakuwa wamedhaminiwa na serikali hivyo ni vyema kutumia dhamana hiyo kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.

Amesema: “Kutumia vocha hizo tofauti na madhumuni kunapunguza uwezo wa Taifa kujitosheleza kwa chakula licha ya kuwa ni haki ya mkulima na sio upendeleo kupata vocha hizo hivyo itumike ipasavyo katika kuongeza uzalishaji wa mazao husika.”

Ameeleza kuwa vocha 2,999,778 za pembejeo za kilimo zenye dhamani ya 78,054,970,000 zimesambazwa katika mikoa 24 (Dar es salaam haipo) ya Tanzania bara kwa ajili ya kufidia gharama za mbolea na mbegu bora katika msimu wa kilimo wa 2015-16 ambazo zitawanufaisha wakulima 999,926 wa mahindi na mpunga.

Kasuga amesema majukumu ya utekelezaji wa mfumo huo wa pembejeo yamegawanywa katika ngazi sita ambazo ni, Wizara Kilimo Chakula na Ushirika, Kamati ya Taifa ya uendeshaji wa uratibu wa vocha, mikoa, wilaya, kata na vijiji.

Amesema kuwa majukumu ya ngazi zote ni pamoja na kutoa elimu ya usimamizi na utekelezaji wa ruzuku ya pembejeo kwa wakulima, kutambua kaya za kilimo zinazonufaika, kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa mpango wa ruzuku kwa kutumia vocha.

“Makampuni 23 ya mbolea na 27 ya mbegu bora ya mahindi na mpunga yanaendelea kutoa huduma ya usambazaji wa pembejeo katika mikoa husika,” amesema Kasuga.

error: Content is protected !!