November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakulima watakiwa kuchangamkia Kampeni ya ‘Vuna Zaidi Na NBC Shambani’

Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw Abdallah Malela (wa kwanza kushoto) akikabidhi zawadi ya guta kwa mmoja wa washindi wa droo ya nne ya kampeni ya Vuna Zaidi na NBC Shambani inayoendeshwa na Benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara, Bw Ally Ismail ambae ni Katibu Mkuu wa AMCOS ya Tangazo iliyopo Mkoani Mtwara wakati wa hafla ya ya kukabidhi ya zawadi mbambali kwa washindi wa kampeni hiyo iliyofanyika mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kusini Bi Zubeider Haroun(Kushoto) na Meneja wa Benki hiyo tawi la Mtwara Bi Editha Mwakatobe (wa pili kushoto)

Spread the love

 

Serikali mkoani Mtwara imesema ipo tayari kuonesha ushirikiano zaidi na taasisi pamoja na wadau mbalimbali wenye nia thabiti na mipango inayolenga kuwasaidia wanachi katika kuleta maendeleo na kuwakwamua katika umaskini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Akizungumza mwishoni mwa wiki mkoani humo wakati wa mnada wa korosho uliombatana hafla fupi ya kukabidhi ya zawadi mbambali kwa wakulima wa korosho mkoa wa Mtwara walioibuka washindi wa droo ya nne ya   kampeni ya ‘Vuna Zaidi na NBC Shambani’ Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw Abdallah Malela alitolea mfano ushirikiano uliopo baina ya viongozi wa serikali  mkoani humo na benki ya NBC unaosababishwa na namna benki hiyo ilivyo mstari wa mbele katika kuchochea maendeleo sambamba na kuwahudumia vyema wakulima hususani wa zao la korosho.

 Kwa upande wake Meneja wa Benki ya NBC tawi la Masasi Bw Eric Mbeyale alisema kupitia droo hiyo ya nne benki ilitoa zawadi za aina mbalimbali kwa washindi ikiwemo pikipiki, baiskeli, pampu za kupulizia dawa  mikorosho, guta,  pamoja na zawadi za nyingine  ikiwemo kanga, mabegi ya shule na madaftari kwa wakulima mmoja mmoja na AMCOS katika mikoa ya Mtwara na Lindi.

Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw Abdallah Malela (wa pili kushoto) akikabidhi zawadi ya pikipiki kwa mmoja wa washindi wa droo ya nne ya kampeni ya Vuna Zaidi na NBC Shambani inayoendeshwa na Benki ya NBC mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara, wakati wa hafla ya ya kukabidhi ya zawadi mbambali kwa washindi wa kampeni hiyo iliyofanyika mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw Dunstan Kyobya (kushoto), Meneja wa Benki hiyo Kanda ya Kusini Bi Zubeider Haroun(Kulia) na Meneja wa Benki hiyo tawi la Mtwara Bi Editha Mwakatobe (wa pili kulia)

Kwa upande wao washindi wa droo hiyo waliishukuru benki ya NBC kwa kuandaa kwa kampeni hiyo kwa kuwa imekuwa na msaada mkubwa kwao.

error: Content is protected !!