Tuesday , 21 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wakulima wapewa dawa na mbegu feki
Habari Mchanganyiko

Wakulima wapewa dawa na mbegu feki

Spread the love

JUMLA ya Maofisa Kilimo kutoka katika Wilaya mbalimbali na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wamepatiwa mafunzo na kuwa wakaguzi walioidhinishwa ili kudhibiti matukio ya mbegu feki yanayojitokeza mara kwa mara katika mikoa hiyo na nchi nzima kwa ujumla. Anaripoti Christina Haule … (endelea).

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI), Partick Ngwediagi amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya utaalamu wa mbegu, sheria na kanuni zake kwa maofisa Kilimo kutoka Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika mkoani hapa.

Ngwediagi amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha maofisa kilimo hao wanaiva na kuwa wakaguzi walioidhinishwa baada ya kutangazwa na Serikali kwenye gazeti la Serikali kupitia kwa Waziri mwenye dhamana .

Aidha amesema kuwa kwa sasa kuna wakaguzi wa mbegu walioidhinishwa 200 katika Halmashauri na wilaya zote nchi nzima ambapo kila Halmashauri inapaswa kuwa na wakaguzi walioidhinishwa wawili ili kutekeleza jukumu la ukaguzi wa mbegu.

Amesema kufuatia mikoa hiyo kuwa ndiyo inayofanya shughuli nyingi zinazohusiana na mbegu ikiwemo uzalishaji wa mbegu na uuzaji TOSCI imeona mapungufu ya wakaguzi hao walioidhinishwa na hivyo kuwapa elimu wakaguzi wapya kwa lengo la kupata mbegu na uzalishaji wa mbegu ulio bora huku wakipambana na matukio ya mbegu feki yanayojitokeza katika maeneo hayo mara kwa mara.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa TOSCI, Dk. George Swella aliitaja mikoa wanayotoka washiriki wa mafunzo hayo kuwa ni pamoja na Iringa, Rukwa, Ruvuma, Njombe, Mbeya, Songwe na Katavi ambapo amesema kupitia elimu hiyo anaimani wakaguzi hao wataenda a kupatiwa mafunzo watatangazwa kuwa wakaguzi wa mbegu kwa niaba ya TOSCI katika kila wilaya lengo ni kuhakikisha wanathibiti ubora wa mbegu.

Aidha amesema kuwa wameamua kutoa mafunzo kwa maofisa ugani hao kufuatia mikoa hiyo ya Nyanda za Juu Kusini kuwa ndio kitovu cha chakula nchini ambapo wamegundua katika mikoa hiyo maofisa kilimo wengi wamefukuzwa, wamestaafu au wameacha kazi na kubakiza mapengo yanayoenda kuzibwa kwa sasa.

Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Florence Kaaya kutoka Halmashauri ya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma amesema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha kufanya kazi kwa ufanisi ikiwemo kudhibiti na kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa mbegu bora ambazo watanzania wataenda kuzitumia na kuongeza uzalishaji na kuepukana na mbegu feki.

Taasisi ya uthibiti ubora wa mbegu Tanzani (TOSCI) ni taasisi iliyo chini ya Wizara ya kilimo ambapo ilianzishwa kwa mujibu wa sheria ya mbegu namba 18 ya mwaka 2003.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tanzania yakabidhi rasmi msaada nchini Malawi

Spread the loveWAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,...

Habari Mchanganyiko

Bashe: Tumeshagawa pikipiki 5,500 kati ya 7,000 kwa maafisa ugani

Spread the love  WAZIRI wa Kilimo, Hussen Bashe, amesema wizara hiyo tayari...

Habari Mchanganyiko

Spika Tulia awapa neno mawaziri utekelezaji mashamba ya pamoja

Spread the love  SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri kushirikiana...

Habari Mchanganyiko

Ukosefu wa maadili kwa wakunga, wauguzi bado changamoto

Spread the loveIMEELEZWA kuwa vitendo vya uvunjifu wa maadili kwa  wauguzi na...

error: Content is protected !!