
Shamba la mpunga
WAKULIMA wa zao la Mpunga nchini wameshauriwa kuendesha kilimo cha umwagiliaji kinachojulikana kama kilimo Shadidi ambacho kina matumizi madogo ya maji na uzalishaji wake ni mkubwa ikilinganishwa na umwagiliaji wa aina nyingine. Anaandika Kenneth Ngelesi … (endelea).
Wito huo umetolewa na Mtaalamu wa Kilimo cha Umwagiliaji Mnadi Taribo kama moja ya mbinu za kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi katika kipindi hiki ambapo msimu wa mvua umebadili msimu wa kilimo cha mazao mbali mbali na hivyo kuathiri uzalishaji wa mazao hayo.
Taribo amesema hayo alipokuwa akizungumza na Jukwaa la Wadau wa Mazingira katika mkutano ulioandaliwa na Bodi ya maji ya Bonde la Ziwa Rukwa ambalo limelenga kujadili mabadiliko ya tabia ya nchi na athari zake katika maisha ya kila siku na namna ya kukabiliana na tatizo hilo.
Mkutano huo ulifanyika Jijini Mbeya Taribo amesema zao hilo ni moja ya mazao ya chakula na biashara kwa wakulima wa hapa nchini, kwa muda mrefu kilimo hiki kimekuwa kikitumia umwagiliaji kwa njia ya Faro, Misingi na nyinginezo za asili ambazo zilikuwa na tija kulingana hali ya hewa tofauti na sasa ambapo rasilimali maji ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji katika uzalishaji.
Mtaalamu huyo wa kilimo cha umwagiliaji amesema kinatumia gharama katika uhudumiaji wa shamba lakini uzalishaji wake ni mkubwa wa kati ya tani 4 mpaka 11 kwa ekari na kinapunguza asilimia hamsini ya matumizi ya maji ikilinganishwa na umwagiliaji wa aina nyingine.
Mkurugenzi wa Bodi ya maji katika Bonde hilo, Florence Mahai amesema athari za mabadiliko ya tabia ya nchi zimekuwa zikiongezeka siku hadi siku hivyo ni wajibu wa wadau na hasa jumuiya za watumia maji kuendelea kushirikiananna katika kuvitunza vyanzo vya maji.
More Stories
Takukuru yavimbia wakandarasi, ‘yarejesha’ mil 420 Tanesco
IGP Sirro: Hatufungui kesi za madai, migogoro ya ardhi
Panyabuku waanza kubaini TB