Monday , 29 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wakulima korosho wanatudai Bil 50 tu – Serikali
Habari za Siasa

Wakulima korosho wanatudai Bil 50 tu – Serikali

Spread the love

SERIKALI imeeleza, bado inadaiwa kiasi cha Sh. 50 bilioni na wakulima wa zao za korosho. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea). 

Akizungumza na wanahabari leo tarehe 20 Septemba 2019, Japhet Hasunga, Waziri wa Kilimo amesema serikali ilikuwa inadaiwa zaidi ya Sh. 720 bilioni na kwamba imelipa na kusalia 50 bilioni.

“Serikali ilikuwa inadaiwa zaidi ya Sh. 720 bilioni na wakulima wa korosho, mpaka sasa bado tunadaiwa Sh. 50 bilioni. Bado malipo yanaendelea, hivi ninavyoongea inawezekana deni limepungua.

“Tunauza korosho na hela zinazopatikana tunalipa wakulima hela yao kwanza. Kipaumbele chetu ni kuhakikisha mkulima analipwa ili apate fedha za kuandaa mashamba,” amesema Hasunga.

Hasunga ameeleza kwamba, serikali itawalipa wakulima fedha zao zote kabla ya msimu mpya wa korosho haujaanza.

Amesema hadi sasa kuna kampuni takribani 15 zinanunua korosho hizo, na kuwa serikali ikipata fedha itawalipa kwanza wakulima.

Korosho zilikuwepo tani 2240000 kati ya hizo 2129 ziliuzea katika mnada wa awali, zile 222000 kiasi tumebangua ndani zingine tunaendelea kuuza.

“Kuhusu biashara ya sasa hivi inayoendelea ni kweli mimi nimesikia kwamba zote zimeuzwa lakini kwa mujibu wa mkataba wa makubaliano kuna kampuni kama 15 zinazonunua korosho na kila kampuni utaratibu wake ni kwamba mzigo ukiingia kwenye meli zinafanya malipo.

Ni sh ngapi kuna kamati maalumu inayosimamia zoezi la uuzaji pia tuna wizara ya viwanda na biashara ndio kazi yao. Mimi kazi yangu ni kusimamia uzalishaji na ukusanyaji na nishaimaliza.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yaanika madudu miradi ya ujenzi, moundombinu

Spread the loveCHAMA cha ACT Wazalendo kimeeleza wasiwasi juu ya uelekeo wa...

Habari za Siasa

Samia ashuhudia utiaji saini ujenzi wa minara 758 ya bilioni 265

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa kampuni za...

error: Content is protected !!