Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya Wakufunzi wa mikoa wapatiwa mafunzo ya kujikinga na Ebola
Afya

Wakufunzi wa mikoa wapatiwa mafunzo ya kujikinga na Ebola

Spread the love

 

WAKUFUNZI wa mikoa nchini ambao ni wataalamu wa afya kutoka katika hospitali ya Taifa, hospitali za kanda, hospitali maalumu na hospitali za Rufaa za Mikoa, wamepatiwa mafunzo ya kujikinga na ebola. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).

Mratibu wa Mafunzo hayo Dk. Erick Richard amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwatayarisha wakufunzi hao kukabiliana na Ebola na wanaporudi kwenye Mikoa yao kwenda kutoa elimu hiyo kwa watoa huduma ya Afya.

“Wakufunzi hawa tumewafundisha jinsi ya kutambua na kutibu pamoja na kuweza kutumia afua mbalimbali za kujikinga ili waweze kumhudumia mgonjwa wa Ebola pindi anapogundulika bila ya wao kupata maambukizi,” amesema Dk. Richard.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO), yameleta wataalamu wa magonjwa ya Milipuko kutoka nchi ambazo zilishawahi kutokea kwa mlipuko wa Ebola ikiwemo nchi ya Congo DRC, Zambia, Bukinafaso, Cameron, Sierra-Leone kuja kutoa mafunzo hayo nchini.

“Ugonjwa huu hadi sasa haujaingia nchini lakini tumejiandaa na mafunzo haya kuwa ni sehemu ya utayari katika kujijengea uelewa kwa kuujua ugonjwa wa Ebola na kuutibu, kujikinga na maambukizi na kuzuia maambukizi hayo yasisambae,”amesema Dk. Richard

Miongoni mwa mambo waliyofundishwa ni pamoja na kuvaa na kuvua vifaa kinga vya kujikinga na Ebola kwa wahudumu, kupata uelewa wa ugonjwa wa Ebola, Jinsi ya kunawa mikono kwa usahihi, mafunzo kwa vitendo namna ya kumpokea mgonjwa wa Ebola na kumhudumia.

Mafunzo hayo yamemalizika kutolewa kwa mikoa yote 28 Tanzania Bara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

AfyaHabari Mchanganyiko

Wanavijiji wajenga zahanati kukwepa umbali mrefu kupata huduma

Spread the loveWANAVIJIJI wa Kata ya  Musanja Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani...

AfyaTangulizi

Wanasayansi wagundua teknolojia ya kunyofoa VVU kutoka kwenye seli

Spread the loveTIMU ya wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha Amsterdam cha nchini...

Afya

Wananchi 530,000 kufaidika na ujenzi wa hospitali ya bil. 1.8

Spread the love  SERIKALI imetoa Sh 1.8 bilioni kwa ajili ya ujenzi...

error: Content is protected !!