Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Wakopaji watakiwa kutumia mikopo kwa maendeleo
Habari Mchanganyiko

Wakopaji watakiwa kutumia mikopo kwa maendeleo

Mwenyekiti wa KKKT Arusha Road Saccos Ltd, Ibrahim Sumbe
Spread the love

WANACHAMA ambao wapo kwenye vikundi vya hiari vya kukopeshana SACCOS wameshauriwa kutumia fedha wanazokopa kwa ajili ya Maendeleo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Licha ya kushauriwa hivyo wakopaji wote nchini wametakiwa kuhakikisha wanakopa wanarejesha fedha hizo kwa wakati ili kutoa nafasi kwa wanachama wengine kukopa.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa KKKT Arusha Road Saccos Ltd, Ibrahim Sumbe, alipokuwa akisoma taarifa ya Mkutano Mkuu wa kawaida wa mwaka 2019.

Sumbe alisema kuwa Saccos nyingi zinakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo wanachama wa Saccos hizo kukopa fedha na kushindwa kurejesha kwa wakati na kusababisha kuwepo kwa usumbufu kati ya wafuatiliaji wa Mikopo na wanachama.

Akizungumzia kuhusu KKKT Saccos Ltd amesema kuwa licha ya Daccos hiyo kufanya vizuri kwa kufuata miongozo ya uendeshaji bado inakabiliwa na changamoto ya ucheleweshwaji wa Mikopo.

“Chama chetu kina wanachama wachache wanaochelewesha marejesho yao ya mikopo,tunawaomba wanachama wote mjitahidi kuwa waaminifu na mrejeshe mimopo yenu kwa wakati.

“Kwani kwa kutorejesha Mikopo hiyo mnakiretea chama hasara,na chama kitashindwa hata kuwalipa nauli za mikutano wanachama ambao wanachelewesha marejesho yao,” ameeleza Sumbe.

Katika taarifa yake Sumbe amesema kuwa KKKT Saccos Ltd kina wanachama 569 ambapo ukaguzi wa hesabu za chama hicho ufanyika kila mwaka na wakaguzi kutoka COASCO.

Kwa upande wake Mkaguzi wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika,COASCO Mkoa wa Dodoma,Dorah Meta amesema kuwa KKKT SACCOS Ltd amesema Saccos hiyo inafanya vizuri na kusababisha kupata hati safi.

Dorah amesema ushirika huo umekuwa ukifanya kazi zake vizuri kwa kufuata sheria,kanuni na taratibu za uendeshaji wa shughuli za vyama vya ushirika.

Pamoja na kuonekana kwa utendaji mzuri wa Saccos hiyo bado kunachangamoto kubwa katika kipengele cha mikataba kati ya Saccos hiyo na watumishi jambo ambalo bado linatakiwa kufanyiwa kazi.

Jambo lingine ambalo alilisisitiza Dorah ni kuwataka wanachama kuhakikisha wanalipa madeni kwa wakati ili kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza na kusababisha Saccos inafanya vibaya.

Kwa kwa upande wake Witness Msuya ambaye alikuwa Mwenyekiti wa muda katika mkutano huo ametaka uongozi kuhakikisha unafuatilia madeni huku akiwataka wanachama wote kuwa waaminifu na kuwafuatilia wale waliokopa ukizingatia waliokopa wamedhaminiwa na wanachama wenzao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Habari Mchanganyiko

Somo la dini: Waislamu waishukia Serikali, wizara yatoa kauli

Spread the loveJUMUIYA na Taasisi za Kiislamu Tanzania, imetupia lawama Serikali ikidai...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!