December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakili wa Nondo awageuzia kibao Polisi

Spread the love

JESHI la Polisi limetakiwa kufanya upelelezi wa waliohusika kumteka Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Wito huo umetolewa na Wakili aliyekuwa anamtetea Nondo katika kesi ya kujiteka, Wakili John Sendodo wakati akizungumza na wanahabari leo tarehe 7 Novemba 2018.

Nondo alishitakiwa kwa kesi ya msingi ya kudanganya kuwa alitekwa na kutoa taarifa za uongo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, kesi ambayo alishinda baada ya mahakama kumkuta hana hatia kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yake.

“Tunalitaka Jeshi la Polisi kuanza upelelezi wa watekaji waliohusika na utekaji wa Nondo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria,” amesema Wakili Sendodo.

Katika hatua nyingine, Mtandao wa Utetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umevitaka vyombo vya dola kuacha kuwakamata watetezi wa haki za binadamu wanapotekeleza majukumu yao na kuwafungulia kesi badala yake kuungana nao katika kuifanya kazi ya utetezi.

“Baadhi ya Viongozi nchini waache kulitumia Jeshi la Polisi kwa kutoa maagizo yanayokwenda kinyume na sheria na utawala bora, Jeshi la Polisi linapaswa kuwa huru na kujitegemea katika kufanya kazi zake,” inaeleza sehemu ya tamko lililotolewa na THRDC.

error: Content is protected !!