Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wakili wa Mbowe, Jamhuri watoana jasho
Habari za Siasa

Wakili wa Mbowe, Jamhuri watoana jasho

Freeman Mbowe, Kiongozi wa Chadema (wa pili kulia) na wenzake wakiwa mahakamani Kisutu
Spread the love

UPANDE wa Jamhuri umewasilisha hoja zao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, juu pingamizi la upande wa utetezi kuhusu kupokelewa kwa kielelezo cha kamera na tape mbili za video, kwenye ushahidi wa kesi ya viongozi waandamizi wa Chadema. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Viongozi tisa wa Chadema wanakabiliwa na mashtaka 13 ya uchochezi. Viongozi hao ni pamoja na Freeman Mbowe, Mwenyekiti-Taifa, Dk. Vicent Mashinji Katibu Mkuu; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Bara na Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar.

Wengine ni Ester Matiko, Mhadhini wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha)-Taifa pia Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mwenyekiti wa Bawacha-Taifa pia Mbunge wa Kawe; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini; Peter Msigwa na Mbunge wa Iringa Mjini.

Kwenye shauri hilo, upande wa serikali uliwakilishwa Dk. Zainabu Mango Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi, Faraja Nchimbi, Wankyo Simon, Jackline Nyantori.

Upande wa utetezi umeongozwa na Profesa Abdallah Safari, Peter Kibatala, John Mallya na Hekima Mwasipu.

Jana tarehe 3 Julai mwaka 2019, upande wa utetezi uliwasilisha pingamizi juu ya kupokelewa mahakamani hapo kielelezo cha kamera na tape mbili za kurekodia video.

Kibatala, wakili wa upande huo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba aliwasilisha hoja hizo kwa kudai kuwa, ushahidi wa kieletroniki hauwezi kupokewa mahakamani mpaka kuwepo kwa kiapo mahususi juu ya utoaji wa vielelezo hivyo, kwa mujibu wa sheria fungu la 18 na 19 ya ushahidi wa kieleketroniki.

Upande wa serikali uliomba kuahirishwa kwa kesi hiyo ili uje na majibu ya hoja hizo.

Leo Mahakamani hapo

kwenye kesi hiyo, Dk Zainab Mango, Wakili wa Serikali Mkuu
amedai kuwa, Jamhuri imefanikiwa kukidhi matakwa yote ya ushahidi wa kielekroniki.

“Ni rai ya upande wa Jamhuri, tumefanikiwa kukidhi matakwa yote ya sheria kifungu cha 18 (2) cha sheria ya ushahidi wa kielekroniki yanayotaka vielelezo vitunzwe vizuri kabla kuwasilishwa mahakamani, ambapo shahidi wa Jamhuri jana aliielezea mahakama namna aliyovitunza vielelezo hivyo,” ameeleza Dk. Zainabu.

Amedai kuwa, matakwa ya sheria juu ya ushahidi huo ni pamoja na kutunzwa na kuhifadhiwa kwa vidhibiti vya kielekroniki na mtu akiyehusika kwenye kuchakata vielelezo hivyo, pia vifaa vilivyotumika viwe vizima bila kutumika mahala kwengine.

Dk. Zainabu amedai kuwa, Kifungu cha 18 kinahitaji kitu kitachouthibitishia mahakama juu vielelezo hivyo na kwamba, ushahidi unaweza kutolewa kwa maneno, nyaraka au hati ya kiapo.

Akirejee kesi iliyotajwa na Kibatala jana, ile ya Exim Bank na Kilimanjaro Cofee Company Limited, kesi namba 29 ambayo iliamriwa mwaka 2013 kabla ya marekebishonya sheria ya ushahidi wa kielekroniki na kwamba, kesi hiyo inahusiana masuala ya kibenki na kuwa, sheria yenyewe inasheria mahususi yanayohusu masuala ya benki ambayo ni kifungu cha 78 (A) sambamba na fungu la 79.

Pia akarejea kesi ya Emmanuele Mwasonga ambayo ushahidi wa simu ulikataliwa mahakamani, kutokana namna ulivyohifadhiwa ambapo simu ile iliyorekodi sauti, ilimrushia mtu mwengine na baadaye ile simu iliyorekodi kupotea huku sauti ikiweka kwenye CD na baadaye kupelekwa mahakamani, ilikuwa sababu ya kukataliwa.

Paul Kadushi, Wakili wa Serikali Mkuu ameieleza mahakama kuwa, ushahidi uliotolewa umekidhi vigezo na matakwa ya kifungu cha 18 (2), (a), (b) na (c).

Amedai kuwa, matakwa ya sheria ina kigezo cha kifaa kilichohifadhi ushahidi kuwa kinafanya kazi wakati wote.

Kadushi ameeleza mahakamani hapo kuwa, hoja yao ya pili kuwa suala la hati ya kiapo, ushahidi wa kurekodiwa kwenye mashauri ya jinai sheria hakuna hitajio la kisheria linalotaka utolewaji wa ushahidi wa kieletroni utolewa kwa hati ya kiapo, sio kifungu cha 18 wala kifungu kingine chochote.

Kadushi amesisitiza kuwa, katika mashauri ya madai ni jambo la kawaida ushahidi kuwasilishwa kiapo ambapo kwa mashauri ya jinai mahakama inapokea kwa njia ya maneno.

“Sisi tunawasilisha kuwa, kuwepo kwa hati ya kiapo sio hoja, tunaiomba mahakama yako isizingatie kabisa mapingamizi yaliyowasilishwa na wenzetu na ipokee vielelezo vilivyotolewa na shahidi,” amewasilisha Kadushi.

Kibatala akijibu hoja hizo ameendelea kusisitiza kuwa, katika kutoa ushahidi wa kieletroniki licha ya shahidi kutoa ushahidi wake mkuu, lazima kuwepo kwa kiapo mahususi kwa ajili ya kutoa ushahidi wa kieletroniki.

“Sheria ya kieletroniki imelenga hasa mahakama kuu kitengo cha biashara na hata utungwaji wa sheria, hivyo umetokana na mashauri ya kibiashara kwenye mahakama hiyo. Hivyo tunabomoa hoja Dk. Mango kuwa, eti kwasababu uamuzi wa kesi ya Exim Benki umefanywa kabla ya marekebisho ya sheria ya elekriniki, sheria haielei hewani,” amedai.

Kibatala amedai kuwa ushahidi huo ungeweza kukubaliwa kwa mujibu wa sheria labda kutoka kwenye CCTV kamera au kwa Mwandishi wa Habari lakini shahidi huyu anatoka kwao (Jamhuri).

Amedai kuwa tafsiri ya ‘au’ ‘na’ (‘And’ & ‘Or’) kwenye kifungu cha 18 kimetumiwa vibaya na wakili Kadushi na kwamba, hitaji la fungu la 18 (a) na (b) visomwe kwa pamoja kwamba, vielelezo vile vingetolewa endapo vinamilikiwa na washtakiwa.

Mwasipu ameendelea kujibu hoja ameeleza kuwa, shahidi wa sita ni Ofisa wa Polisi aliyekuwa chini ya Ofisi ya Mkuu wa Upulelezi, Mkoa wa Kinondoni ambaye ana maslahi kwenye shauri hilo.

Baada ya kuwasilisha majibu hayo, Hakimu Simba ameiharisha shauri hilo na litasikilizwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 24, 25 na 26 mwezi Julai mwaka 2019 ambapo atatoa uamuzi juu ya pingamizi hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!