Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wakili wa Mbowe alivyombana kwenye ‘kona’ shahidi wa Jamhuri
Habari za SiasaTangulizi

Wakili wa Mbowe alivyombana kwenye ‘kona’ shahidi wa Jamhuri

Viongozi wa Chadema wakiwa Mahakamani Kisutu
Spread the love

BAADA ya shahidi namba saba wa Jamhuri, Victoria Wihenge kumaliza kutoa ushidi wake kwenye kesi ya uchochezi namba 112/2018 inayomuhusu Freeman Mbowe, Mwenyekiti Chadema Taifa na wenzake wanane, alihojiwa na wakili wa utetezi Peter Kibatala. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Kesi hiyo inamuhusu Mbowe, Mwenyekiyi wa Chadema Taifa, Dk.Vicent Mashinji, Katibu Mkuu-Taifa; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu – Bara na Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu -Z’Bar.

Wengine ni Ester Matiko Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Mahojiano yalikuwa hivi:-

Kibatala: Unafahamu hii kesi ni ya kitu gani?

Shahidi: Uchaguzi wa Ubunge jimbo la Kinondoni

Kibatala: Unafahamu hawa washtakiwa wanashtakiwa kwa kutoa maneno ambayo upande wa serikali unaidai ni kinyume na sheria.

Shahidi: Kimya

Hakimu: Rudia kumuuliza.

Kibatala: Unafahamu hawa washitakiwa, wanashtakiwa pamoja na mambo mengine, kwa kutoa maneno ambayo upande wa Jamhuri unaidai ni kinyume cha sheria.

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Shahidi uliitwa kwa summons (wito wa mahakama) au ulipigiwa simu au mtu alikuja ofisini kukuona?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu, utaratibu wa kuitwa mahamamani unafahamika.

Kibatala: Narudiwa kama hujanielewa useme.

Shahidi: Kimya.

Kibatala: Utaratibu upi ulitumika ulipewa summons?

Shahidi: Niliitwa na mahakama.

Kibatala: Ulipewa summons?

Shahidi: Kimya.

Kibatala: Ni mara yako ya kwanza leo kutoa ushahidi mahakamani, nafahamu ushawahi kutoa ushahidi mara kadhaa kwenye kesi za uchaguzi. Ni sahihi?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu, sikujua kuwa nakuja kutoa ushahidi bali kutoa elimu.

Kibatala: Ni sahihi ulishawahi kutoa ushahidi katika kesi za uchaguzi mara kadhaa, ni sahihi?

Shahidi: Sio sahihi

Kibatala: Uliitwa kwa utaratibu gani?

Shahidi: Niliitwa kwa njia formal

Kibatala: Shahidi

Hakimu: Naandika anachojibu

Kibatala: Kwa majibu haya, tutaka hadi saa 12.

Hakimu: Hata kama kesho.

Kibatala: Shahidi ulipigiwa simu, kuna barua, mtu alikufuata?

Shahidi: Mheshimiwa aliandikiwa msimamizi kwa barua.

Kibatala: Shahidi, hiyo barua iliyoelekezwa kwa bosi wako mkurugenzi au msimamizi wa uchaguzi, uliiona au hukuiona?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu niliiona.

Kibatala: Ilinakiliwa kwako, haikunakiliwa kwao?

Shahidi: Mheshimiwa sijaelewa

Kibatala:  Ilinakiliwa kwako, haikunakiliwa kwao?

Shahidi: Hapana.

Kibatala: Kwa hiyo msimamizi amekuambia kuna baraua lakini hukuiona?

Shahidi: Mheshimiwa Hakimu, nimepewa maelekezo na msimamizi

Kibatala: Kwa hiyo hukuambiwa kuwa, kesi hii ni ya jinai iliyotokana na kampeni za mwaka 2018 tarehe 16 Agosti?

Shahidi: Kimya

Kibatala: Shahidi nikufafanunulie au pozi zako

Hakimu: Mwenzetu sio mwanasheria

Kibatala: Jana wakati unakuja kutoka kwako, ulifahamu unakuja kutoa ushahidi katika kesi gani?

Shahidi: Sikufahamu

Kibatala: Shahidi nakuosomea maneno yapo kwenye hati ya nne, Ninapozungumza hapa kiongozi wetu wa Hananasif yupo Monchwari amekamatwa na Makada wa CCM kwa msaada wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wamemnyonga wamememua .. Halafu sisi tunaonajambo la kawaida tunacheka na Polisi tunacheka na CCM.

Shahidi: Niliwawahi kusikia kwenye vyombo vya habari.

Kibatala: Ni vyombo vipi?

Shahidi: Mitandao ya kijamii

Kibatala: Hebu itaje hivyo vyombo vya habari au mitandao ya kijamii.

Shahidi: Niliwahi kusikia kwenye mitandao ya kujamii.

Kibatala: Twitter au Instagram?

Shahidi: The same.

Kibatala: Ipi?

Shahidi: Instergra.

Kibatala: Mwambie hakimu, kwenye page (kurasa) ya nani?

Shahidi: Siwezi kukumbuka

Kibatala: Ilikuwa lini uliyasikia hayo maneno mwaka gani mwezi gani?

Shahidi: Ni kipindi cha uchaguzi wa mbunge jimbo la Kinondoni

Kibatala: Kabla ya uchaguzi au baada ya zoezi la uchaguzi?

Shahidi: Naposema kipindi cha uchaguzi, namaanisha tarehe 10 Januari 2018 hadi tarehe Februari tarehe 17, 2018.

Kibatala: Kati ya tarehe 10 Januari na 17 Februari 2018, kikao cha kamati ya maadili kilikaa mara ngapi?

Shahidi: Kilianza tarehe 20.

Kibatala: Nakuuliza vizuri, kati ya tarehe 10 Januari 2018 na 17 Februari 2018 vilikaa mara ngapi?

Shahidi: Vikao vilianza tarehe 20 Januari 2018.

Nchimbi: Msikilize Wakili anachokuuliza.

Hakimu: Afadhali Nchimbi umeelekeze shahidi yako kama unajua unasema unajua, kama hujui unasema hujui. Hatutoi maksi hapa.

Kibatala: Kazi ya kamati ya maadili nini?

Shahidi: Kushughulikia malalamiko ya uvunjwaji wa maadili.

Kibatala: Tusaidie, namna kamati ya maadili iliyokuwa ikisimamia ilikuwa inapokeaje malalamiko.

Shahidi: Malalamiko yalikuwa yanapokelewa kutoka kwa wadau wa uchaguzi.

Kibatala: Ni sahihi uchaguzi wanajumuishwa wananchi?

Shahidi: Nilisema, wadau wa vyama vya siasa. Ni vyama vya siasa

Kibatala: Kwa hiyo wananchi sio wadau wa uchaguzi, sahihi?

Shahidi: Sahihi… mheshimiwa hakimu wananchi ni wadau wa uchaguzi

Kibatala: Ni sahihi wananchi wa jimbo la Kinondoni wanaweza kuleta malalamiko?

Shahidi: Mheshimiwa wenye kuleta ni vyama vya siasa wakiwakilisha wananchi.

Kibatala: Mwananchi hana haki ya kupeleka malalamiko

Shahidi: Mwanachi wa kawaida hawezi.

Kibatala: Mwambie hakimu, kwa sheria ipi inamzuia mwananchi?

Hakimu: Amesema mwananchi wa kawaida

Kibatala: Natumia neno mpiga kura, ni sheria ipi inamzuia mpiga kura wa jimbo la Kinondoni kupeleka malalamiko yake?

Shahidi: Maadili ya tume ya uchaguzi.

Kibatala: Ni sahihi watu pekee kwa ushahidi wako wanaopaswa kutoa malalamiko ni wanasiasa, na maofisa wa tume?

Shahidi: Ndio mheshimiwa

Kibatala: Kumbukumbu za kikao cha maadili zinatunzwa vipi?

Shahidi: Muhtasari.

Kibatala: Je, Chama cha Wananchi (CUF) kiliwahi kupeleka maneno niliyoyasoma kwenye kamati ya maadili?

Shahidi: Mheshimiwa hakimu, sijui

Kibatala: Katika vyama unavyosema 11 ukitoa Chadema, ni chama kipi kiliwahi kupeleka malalamiko kwenye kamati ya maadili kuhusiana na uchaguzi wa Kinondoni?

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Ni sahihi moja wapo ya adhabu inayotolewa kwa chama ni kuzuiwa yeye binafsi au chama kushiriki zoezi la uchaguzi?

Shahidi: Sio sahihi

Kibatala: Jana ulitaja kifungu 102?

Shahidi: Sikutaja kifungu chochote jana.

Kibatala: Mhehimiwa hakimu, tukumbushe kwenye maelezo yake ya jana

Hakimu: Anapekua

Kibatala: Alitaka kifungu cha maadili kati ya 102 au 112, eneo lenyewe alisema kuwa, msaidizi msimamizi anakuwa mwenyekiti na wajumbe wengine wanatoka kwenye vyama vya siasa.

Hakimu Simba: Anarejea maelezo ya jana amesema, haipo kwenye rekodi

Kibatala: Kwa ufahamu wako, sheria haitoi adhabu kwa mgombea ua chama kitakachokiuka maadili ya uchaguzi?

Shahidi: Hapana

Hakimu: Nishamrekodi

Kibatala: Shahidi ni sahihi kwa mgombea au chama kuzuiwa kushiriki kwenye uchaguzi?

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Je kati ya tarhe 10 Januari 2018 na 17 Februari 2018 kamati ya maadili ilitoa adhabu kwa maneno hayo niliyosoma kwa mgombea au chama cha Chadema?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mwambie hakimu, iwapo unaipenda au unaichukia CCM?

Shahidi: Sina Jibu

Kibatala: Ni sahihi shahidi ofisa wa uchaguzi kama wewe anakatazwa kuwa na mahaba au husada kwa chama cha siasa?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Shahidi ni sahihi pia hufahama katazo hilo lipo kwenye kifungu gani juu msimamizi wa uchaguzi kuwa na mapenzi au husuda na vyama vya siasa

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Na wewe umesema ofisa wa ngazi gani? tukumbushe

Shahidi: Ofisa Uchaguzi

Kibatala: Na ni wewe ndiye nchi ya Tanzania imekuamini umsaidie Mkurugenzi kwenye uchaguzi jimbo la Kinondoni

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Tutajie majina ya mkurugenzi wako?

Shahidi: Aron Kamgurujili.

Kibatala: Shahidi wewe ni msomi katika Chuo cha Deplomasia, hujui jina la bosi wako (amelitaja).

Kibatala: Shahidi, wewe ni msomi katika Chuo cha Deplomasia, hujui jina la bosi wako ambalo ni Kagunumujuli

Kibatala: Shahidi unazifahami alama za Chama Cha Mapinduzi?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Ni sahihi alama ya CCM ni T-shirt (fulana) ya kijani na njano?

Shahidi: Naposema alama ni ile ninayoiona kwenye nyaraka za uchaguzi

Kibatala: Unafahamu rangi za mavazi ya Chama Cha Mapinduzi?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Unafahamu rangi za mavazi ya wafuasi wa Chadema?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Unasema, ulikiwa msimamizi wa uchaguzi Kinondoni kwa miaka mingapi

Shahidi: Tangu 2016

Kibatala: Kwa ruhusa yako, nimsimamishe John Heche huyu mavazi aliyovaa unayafahamu? (amevaa kombati ya kaki)

Shahidi: Ndio kwa kuwa kuna nembo.

Kibatala: Unalichukia jeshi la polisi?

Shahidi: Sina maoni

Kibatala: Na Serikali?

Shahidi: Sina maoni

Kibatala: Nimekuuliza kuwa na mahaba au laana na jeshi la polisi na serikali ya Jamhuri pamoja kwamba uliyasikia maneno, ni sahihi huna maoni pamoja na kusikia maneno haya?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Ni sahihi kwamba wewe ni mwananchi wa kawaida wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Shahidi: Ndio mheshimiwa

Kibatala: Kabla sijakupeleka kwenye shitaka la tano, nashika simu yangu naangalia majina kadhaa, naomba umwambie majina ya mgombea wa Chadema

Shahidi: Nakumbuka ni mwalimu

Kibatala: Wewe ndiye uliyesimamia uchaguzi huo, jina la kwanza unalikumbuka au hulikumbuka?

Shahidi: Hilo ndio ninalolikumbuka.

Kibatala: Jina la pili la mgombea wa CCM

Shahidi: Mtulia

Kibatala: Labda nikuulize hivi, kwamba ulilitaja kwa ufasaha jina la mgombea wa CCM wakati unatoa ushahidi wako?

Shahidi: Nilitaja

Kibatala: Kwa hiyo, awali ulitaja sasa hivi hukumbuki sio ndio?

Shahidi: Kimya

Kibatala: Nimepozi kwa sababu shahidi ameagiza maji.

Hakimu: Muulize

Kibatala: Toka wakili wa serikali akuulize maswali, zimepita dakika ngapi?

Shahidi: Zaidi ya masaa matatu

Kibatala: Ni sahihi au sio sahihi kumbukumbu zako zinapotea kwa masaa matatu?

Shahidi: Sio sahihi.

Kibatala: Kama nilivyosema nipo kwenye eneo la ufahamu wako, nitakutajia majina kadhaa kabla sijakutajia ni wagombea wangapi walishiriki kwenye uchaguzi wa jimbo la Kinondoni?

Shahidi: Nilisema 11

Kibatala: Shahidi nakuuliza ni wagombea 11 au 12 walishiriki uchaguzi wa jimbo la Kinondoni?

Shahidi: 11

Hakimu: Kumywa maji dada

Kibatala: Kwa hiyo unasema 11 ukiwa chini ya kiapo na wewe ukiwa ofisa uchaguzi ni sahihi?

Shahidi: Ofisa uchaguzi.

Kibatala: Wewe ni mtu sahihi au sio mtu sahihi kuhusiana na kukumbuka idadi ya wagombea jimbo la Kindondoni?

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Ali Abdallah wa Tadea alipata kura 97, unamfahamu au humfahamu?

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Ashiri Kiwendu AFP unamfahau?

Shahidi: Simfahamu nina maana simkumbuki.

Kibatala: Shahidi kwa mujibu wa fomu aliyopewa Salum Mwalimu iliyosainiwa na bosi wako, wagombea wapo 12, nakuuliza kwa mara ya tatu na ya mwisho, fomu hiyo iliyojazwa wagombea ni 11?

Shahidi: Mimi nawatambua wagombea 11

Kibatala: Kwa ruhusa ya mahakama nakuonesha nyaraka fulani hapa halafu uieleze mahakama, unamfahamu huyu aliyekuwepo kwenye picha hii (alimuonesha picha yake aliyevaa skafu ya njano na kijani)?

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Mtu huyu sio wewe

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Shahidi unafahamu au hufahamu bosi wako walikuwa ni moja kati ya watu waliotajwa Mahakama Kuu kweye kesi iliyofunguliwa na Bob Chacha Wangwe iliyoamuriwa na Mahakama kuu kuwa yeye ni kada wa CCM.

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Unafahamu uwepo wa hukumu hiyo au hufahamu

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu uwepo wa uamuzi watu kama boss wako wasisimamie uchaguzi kwa kuwa ni makada

Shahidi: Sio sahihi ni wateule.

Kibatala: Wateule wa nani

Shahidi: Wa rais

Kibatala: Ni sahihi kuwa Boss wako ndio msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la kinondoni .

Hakimu: Rudia swali

Kibatala: Ni sahihi kuwa Boss wako ndio msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la kinondoni

Shahidi: Mheshimiwa hakimu aulize swali kama alivyouliza mwanzo

Kibatala: Amerejea

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi hukumu ya Mahakana kuu imesomwa baada boss wako kusimamia uchaguzi wa jimbo la Kinondoni?

Shahidi: Sio sahihi.

Kibatala: Nitajie mwaka gani hukumu hiyo imesomwa

Shahidi: Sina uhakika.

Kibatala: Unawezaje kusema kuwa kesi hiyo imekuja baada ya bosi wako kusimamia uchaguzi?

Shahidi: Baada ya uchaguzi mkuu wa 2015.

Kibatala: Sio jibu

Nchimbi: Ndio jibu la swali

Kibatala: Unawezaje kusema kesi imekuja baada ya bosi wako kusimamia uchaguzi

Shahidi: Nimesema uchaguzi wa mwaka 2015 ni vitu viwili tofauti na uchaguzi wa mwaka 2018.

Kibatala: Form four ulipata division ngapi

Shahidi: Three.

Kibatala: Ya ngapi?

Shahidi: 25

Kibatala: Baada hapo.

Kibatala: Unamtambua Salum Mwalimu?

Shahidi: Ndio.

Kibatala: Uliongozwa kumtambua?

Shahidi: Sikuongozwa.

Kibatala: Mtu akitaka kujua kuwa mtu fulani aligombea ubunge?

Shahidi: Fomu namba 9b.

Kibatala: Na kitu kingine ni barua ya chama?

Shahidi: Sahihi.

Kibatala: Hizo fomu namba 9 na barua ya kumtambulisha umezitoa au hujazitoa?

Shahidi: Siazitoa.

Kibatala: Ni sahihi kuwa hizi nyaraka mbili hujawahi kuzifanyia kazi?

Shahidi: Sijawahi kuzifanyia kazi nimeziona.

Kibatala: Ni nani mtunzaji wa kisheria rasmi wa hizo fomu wewe au Bosi wake?

Shahidi: Tume ya Uchaguzi.

Kibatala: Ambaye ni nani kwa ngazi ya jimbo?

Shahidi: Wasimamizi wa uchaguzi pamoja na mimi kipindi cha uchaguzi.

Kibatala: Umetoa ratiba ya kampeni mahakamani kwa ushahidi wako wewe kila chama kinapewa ratiba ili kuondoa migongano sasa nataka umwambie hakimu kama umeitoa kama kielelezo.

Shahidi: Ipo imeshaletwa.

Hakimu: Sikiliza swali.

Wakili wa Serikali Nchimbi anaongea na shahidi.

Hakimu: Usimnong’onezee shahidi.

Kibatala: Shahidi umetoa ua hujatoa ratiba kama kielelezo.

Shahidi: Sijatoa.

Kibatala: Ni sahihi kwamba kamati ya maadili ilikaa mara kadhaa na kuazimia mambo kadhaa.

Shahidi: Sio sahihi.

Kibatala: Mheshimiwa Hakimu, shahidi amesema sio sahihi

Shahidi: Naomba nirekebisha.

Kibatala: Unataka kurekebisha nini.

Shahidi: Vyote viwili.

Kibatala: Swali huwezi

Shahidi: Vikao vya kamati vilikaa.

Baada ya kuahirisha kwa dakika 20, Wakili Kibatala ameiomba Mahakama kuahirisha usikilizaji wa shauri hilo kwa madai kuwa kipande kilichobaki kwa upande wao ni kirefu na kwamba muda umeenda (saa 11 kasoro), pia hoja binafsi kuwa kesho anakesi ndefu Mahakama Kuu kati ya Tundu Lissu aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Spika wa Bunge Job Ndugai.

Nchimbi ameileza Mahakama kuwa hana sababu ya kupinga ombi hilo lakini ameomba shauri hilo liende haraka kwa kuwa shahidi huyo mwisho wa wiki ijayo atakuwa nje ya nchi.

Heche amesimama na kuiomba mahamaka kuwa wiki ijayo atakuwa na majukumu ya kilazima ya kibunge atashindwa kuhudhuria.

Hakimu Simba ameumba upande wa mashtaka kwenda kasi ili kufunga ushahidi licha ya kuwa mahakama haina mamlaka ya kufunga ushahidi ameahirisha shauri hilo mpaka 29, 30 Agosti 2019 na tarehe 10.11 na 12 Septemba 2019.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

Habari za SiasaTangulizi

CAG aibua madudu halmashauri 10, TANESCO na MSD

Spread the loveRIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali...

error: Content is protected !!