Monday , 22 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakili Manyama ajitenga na TLS
Habari MchanganyikoTangulizi

Wakili Manyama ajitenga na TLS

Wakili Leonard Manyama (kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
Spread the love

WAKILI wa kujitegemea ambaye pia ni mwanachama wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Leonard Manyama, amekataa agizo la Rais wa TLS, Tundu Lissu la kuwataka wanachama wake ambao ni mawakili kufanya mgomo kwa siku mbili, anaandika Jovina Patrick.

Lissu alitangaza mgomo huo jana baada ya tukio la kushambulia kwa bomu katika ofisi za IMMMA advocate siku ya jumamosi usiku.

Shambulio hilo linahusishwa na kazi wanazofanya Mawakili hao zikiwamo za kutetea taasisi zinazoishtaki serikali.

Miongoni mwa kampuni ambazo Mawakili hao wanazitetea ni pamoja na ile ya kuchimba madini ya ACACIA ambayo iliingia katika mgogoro baada ya serikali kushikilia mchanga wao uliokuwa ukisafirishwa kwenda nje ya nchi.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Manyama amewataka kuavha kugoma badala yake wafanye zao za kuwasaidia Watanzania wanaowahitaji zaidi kwa wakati huu.

“Viongozi tunapogoma hatuwaumizi tu wahalifu, tunawaumiza hata Watanzania wasio na hatia,” anasema Manyama.

Anasema kuwa wahalifu wana uwezo wa kufanya uhalifu mahala popote na kukumbusha kwamba kazi zao zinawagusa wananchi moja kwa moja.

Lissu alitoa tamko lake baada ya kumalizika mkutano wa baraza la uongozi la chama hicho uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Shambulio la mabomu katika ofisi za mawakili za IMMMA, limezua taharuli na sasa vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi.

“Baraza la uongozi linawataka wanachama wote wa TLS nchi nzima kususia kuhudhuria katika mahakama pamoja na mabaraza ya aina zote kati ya jumanne na jumatano ya tarehe 29 na 30 agost 2017 kwa lengo la kuwaunga mkono mawakili wa Immma advocates.

“Tufanye hivyo ili kuonesha kutokukubaliana kwetu na vitendo vya kuwashambulia mawakili hao kwa mabomu, shambulio dhidi ya wakili mmoja linatakiwa liwe shambulio dhidi ya mawakili wote, IMMMA hawataweza kwenda mahakamani kwa siku kadhaa kwa sababu vitendea kazi vyao vimeharibiwa,”alisema Lissu.

Lissu alisema kuwa mawakili wengine wote nchi nzima wanao wajibu wa kuwaunga mkono IMMMA advocates kwa kutoenda mahakamani vilevile.

Kesi nyingine zinazowakilishwa na mawakili wa IMMMA advocate ni pamoja na kesi ya katibu mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), pamoja na kesi za Tundu Lissu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

Habari Mchanganyiko

DCEA yakamata kilo 767.2 za dawa za kulevya, 21 mbaroni

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!