Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakili apambana kortini kumuokoa Yusuph  Manji 
Habari Mchanganyiko

Wakili apambana kortini kumuokoa Yusuph  Manji 

Yusuph Manji, akizungumza na Wakili wake Hudson Ndusyepo
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo imesikiliza ushahidi wa upande wa serikali kwenye kesi ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya Heroine inayomkabili mfanyabiashara, Yusuph Manji, anaandika Hamisi Mguta.

Ushahidi huo umetolewa mchana huu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha, ambapo shahidi namba moja wa upande wa serikali, Ramadhani Kingai ameiambia mahakama kuwa februali 9, mwaka 2017 akiwa ofisi ya mkuu wa upelelezi kanda ya Dar es Salaam alimpokea mtuhumiwa Manji.

Shahidi huyo ameiambia mahakama kuwa aliagiza mtuhumiwa huyo kupelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali kwa ajili ya vipimo kwa kuwa alituhumiwa kuhusika na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na uuzaji.

Haya ni mahojiano kati ya Wakili wa mtuhumiwa na ofisa wa polisi.

Wakili wa Manji Hudson Ndusyepo: Je  matokeo ya vipimo kutoka kwa mkemia yalionesha Manji anatumia dawa za kulevya aina gani?

Ofisa wa polisi: Dawa za kulevya aina ya Benzodiazepine.

Wakili : Ukiwa kama mkuu wa upelelezi na timu yako mnajua Manji anashtakiwa kwa kosa gani?

Ofisa wa polisi : Ndio kwa kosa la kutumia dawa za kulevya aina ya heroine.

Wakili : Matokeo yaliyokutwa kwenye uchunguzi na ya yaliyopo kwenye mashitaka yana uhusiano wowote?

Ofisa wa polisi :  Mimi siyo mtaalam wa madawa suala hilo linaweza kuelezwa na mtaalam wa madawa ya kulevya.

Wakili : Mlimueleza mtuhumiwa Manji kwamba mnakwenda kumpima mkojo na alijibu nini?

Ofisa wa polisi : Tulimueleza na akakubali kwenda kupimwa.

Wakili: Kama angekataa nini kingefuata?

Ofisa Polisi : Mimi siwezi kujua lakini ninachojua  ni kwamba alielezwa na akakubali kwenda kufanya vipimo.

Shahidi namba mbili wa upande wa mashitaka katika kesi hiyo ni E.1125, Detective Copro, Sospeter.

Shahidi huyo wa pili ameiambia mahakama kuwa februari 9, mwaka huu aliagizwa kumpeleka Manji kwa  mkemia mkuu wa serikali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi kwa sababu alihusishwa na kutumia dawa za kulevya.

Wakili: Maagizo ya kumpeleka Manji kwa mkemia mkuu ulipewa na nani?
Shahidi namba mbili: Nilipewa na kaimu mkuu wa upelelezi, Ramadhani Kingai.

Wakili: Kwa sababu gani?

Shahidi namba mbili : Kwa sababu alihusishwa na kutumia dawa za kulevya.

Wakili : Kabla haujampeleka Manji kumpima ulimueleza ni nini unataka kukifanya?

Shahidi namba mbili : Ndio nilimueleza kwamba tunakwenda kwa mkemia mkuu kufanya vipimo vya mkojo na akakubali.

Wakili: Kabla haujampeleka kwa mkemia mkuu Manji alikaa kwa muda gani kituoni?

Shahidi namba mbili : Mimi sijui, nilichokifabya ni kumpeleka kwa mkemia tu, yaliyofanyika nyuma mimi sifahamu.

Wakili wa upande wa serikali ni Timony Vitalis na shauri hilo litanedelea kesho saa 3 asubuhi mahakamani hapo, na Manji alirudishwa rumande.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

error: Content is protected !!