February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wakenya wabaini  akili za kuambiwa changanya na zako

Raila Odinga, aliyekuwa mgombea wa Muungano wa NASA

Spread the love

WAFUASI wa aliyekuwa mgombea urais nchini Kenya, Raila Odinga wamepuuza kauli yake iliyowataka leo kutoenda kazini, anaandika Victoria Chance.

Odinga aliwataka wafuasi wake kususa kwenda kazini kama ishahara ya kupinga alichodai ni kuibiwa kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliyopita.

Katika uchaguzi huo, aliyekuwa mgombea wa kiti hicho kupitia muungano wa Jubilee, Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi.

Tofauti na hali ilivyokuwa wiki iliyopita, leo maeneo mbalimbali jijini Nairobi ikiwemo mitaa ya Mathare, Kibera wananchi wameanza kufanya shughuliu zao.

Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wamesema  wanahitaji kufanya kazi ili wapate chakula na mahitaji mengine ya msingi huku baadhi yao wakitii kauli ya Odinga.

Aidha, uongozi wa NASA umedai kuwa mitambo ya tume ya uchaguzi haikutenda haki katika kumfanya Kenyatta awe mshindi hivyo wataenda kortini kupinga matokeo hayo.

error: Content is protected !!