Monday , 26 February 2024
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Wakenya kesho kuamua nani awe rais 
Makala & Uchambuzi

Wakenya kesho kuamua nani awe rais 

Uhuru Kenyatta na Raila Odinga
Spread the love

BAADA ya vuta nikuvute za kampeni kali za uchaguzi mkuu nchini Kenya hatimaye wananchi wa nchi hiyo wanatarajia kupiga kura kumchagua Rais na viongozi wengine wa kisiasa, anaandika Hamisi Mguta.

Kuna wagombea wanane katika uchaguzi huo, lakini wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda kiti cha rais ni  Raila Odinga ambaye anatokana na muungano wa National Super Alliance (NASA) na Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee.

Vifaa vitakavyotumika katika kupigia kura kesho Kenya

Uchaguzi huo utafanyika kesho Agost 8 na kampeni zilifungwa jumamosi ambazo zilionyesha waanasiasa hao wawili wakichuana vikali kupitia mikutano ya hadhara.

Taarifa kutoka nchini humo zinasema kwamba unapofanyika uchaguzi mkuu nchini humo, kinachohofiwa siyo nani atashinda bali huyo akayeshindwa kama atakubali matokeo.

Viongozi hao wawili walifanya mikutano miwili ya mwisho siku ya Jumamosi ambayo ilihudhuriwa na maelfu ya watu.

Wakati wa kampeni

Odinga alikuwa kwenye bustani za Uhuru Park, mjini Nairobi, huku Kenyatta akiongoza mkutano wake katika uwanja wa Afraha Stadium, Nakuru, takriban kilomita 160 kutoka Nairobi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Lowassa: Mwanasiasa aliyetikisa CCM, Chadema

Spread the loveWAZIRI Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Edward Lowassa (70) amefariki Dunia...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

error: Content is protected !!