Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakazi Ngorongoro waunda kamati, wamkaribisha Waziri mpya kwa mambo matano
Habari Mchanganyiko

Wakazi Ngorongoro waunda kamati, wamkaribisha Waziri mpya kwa mambo matano

Mwenyekiti wa Viongozi wa Kimila Ngorongoro, Metui Oleshaduo
Spread the love

 

WANANCHI wa Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha, wameunda kamati ya watu 60, kwa ajili ya kushughulikia mgogoro wa ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Taarifa hiyi imetolewa jana tarehe 4 Aprili 2022 na Mwenyekiti wa Viongozi wa Kimila Ngorongoro, Metui Oleshaduo wakati akisoma tamko la kamati hiyo ya mapendekezo, juu ya jitihada za kumaliza migogoro ya ardhi wilayani Ngorongoro.

Oleshaduo amesema kamati hiyo inaongozwa na viongozi wa wilaya akiwemo mbunge, ambayo inajumuisha wawakilishi wa madiwani, wenyeviti, kina mama, viongozi wa kimila na wasomi.

“Kazi kubwa ya kamati hii yenye mchanganyiko wa makundi ya kijamii ni kuwa kiungo kikubwa kati ya wananchi na Serikali, katika kuelekea kutatua migogoro hii bila kuathiri pande zote mbili zinazovutana.

Kamati hii imeanza kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kwa vijiji vyote vinavyozunguka eneo lenye mgogoro wa kilometa za mraba 1,500 pamoja na vijjji vyote vya tarafa ya Ngorongoro,” amesema Oleshaduo.

Oleshaduo amesema, kamati hiyo inatarajia kukamilisha kazi ya ukusanyaji maoni ya wananchi ndani ya muda wa wiki moja, kisha ripoti yake itawasilishwa kwa viongozi wa Serikali na umma.

Katika hatua nyingine, Oleshaduo amesema wanampongeza Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kumbadilisha Waziri wa Maliasili na Utalii, kwa kumtoa Dk. Damas Ndumbaro, na kumuweka Pindi Chana.

Oleshaduo amemtaka Chana kuanza na suala la mgogoro wa Ngorongoro, kwa kuyafanyia kazi mambo matano.

“Pindi Chana aanze na suala la Ngorongoro kwa kufanya haya, kuzuia propaganda zozote dhidi ya wananchi wa Ngorongoro hasa Jamii ya Kimasai.

“Pili kusitisha michakato yote inayoendelea na kutoa nafasi ya kusikiliza jamii, tatu kukataza matishio na kamatakamata yoyote dhidi ya wanajamii, viongozi na watetezi wa haki za binadamu wanaosimama kutetea haki za jamii,” amesema Oleshaduo na kuongeza:

“Kuzuia vitisho dhidi ya waandishi wanaotoa taarifa za umma, tatu kuzuia Wanangorongoro kuitwa si Watanzania, nne kuagiza huduma za msingi ziendelee kutolewa kwa wananchi wa tarafa ya Ngorongoro na tano akutane na kamati hii ili kuanza kujenga mikakati ya pamoja.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!