January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakazi Kijitoupele wakosa kura ya mbunge

Spread the love

WAKAZI wa Jimbo la Kijitoupele, Visiwani Zanzibar wameshidwa kupiga kura ya mbunge kutokana na kutokuwepo karatasi yenye majina ya wabunge wanaopaswa kupigiwa kura. Anaandika Pendo Omary …(endelea).

Wanaogombea katika jimbo hilo ni Shamsi Vuwai Nahodha kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mohamed Juma Aminie anayewakilisha Chama cha Wananchi (CUF) na kuugwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Jabir Idrissa, Mhariri wa gazeti la MwanaHALISI ameiambia MwanaHALISI Online kwamba “katika Jimbo la Kijitoupele mpaka sasa hakuna kura ya mbunge. Tayari waliopiga kura wameondoka. Wasimaizi hawana majibu.”

error: Content is protected !!