January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakazi Dodoma waomba visima kumaliza baa la njaa

Spread the love

ILI kukabiliana na baa la njaa mkoani Dodoma baadhi ya wakazi wa mkoa huo wameiomba Serikali kuwachimbia visima virefu ambavyo vitatumika kwa kilimo cha umwagiliaji pasipo kutegemea kilimo cha mvua. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imeelezwa jana na wakazi wa Mkoa huo katika mahojiano maalumu na MwanaHALISI Online, kuwa nini kifanjike ili kuweza kukabiliana na tatizo la njaa.

Mmoja wa wakazi wa mkoa wa Dodoma Twaha Kivale amesema wananchi wakifanikiwa kupata visima hivyo mkoa utaondokana na baa la njaa ambalo linakabili asilimia kubwa ya wakazi wa mkoa huu.

“Sasa kutokana na hali hii tunaiomba serikali kutuchimbia visima kwani mbali na zabibu ambayo inazalishwa mara mbili kwa mwaka mazao mengine kama mahindi yanaweza kuzalishwa hata mara tatu kwa mwaka,” amesema Kivale.

Hata hivyo alivyoulizwa hukusu wakazi wa Dodoma kudaiwa kuwa ni wa wavivu hawapendi kujishughulisha hali inayodaiwa kuwa chanzo cha tatizo la njaa amesema kuwa ni elimu tu ambayo inatakiwa itolewe kwa wakazi hao.

Kwa upande wake Matika Zakaria mkazi wa Chamwino, amesema serikali imekuwa ikishauri wananchi walime mazao yanayostahimili ukame lakini wananchi wameonekana kukaidi nakuendelea kulima mazao yasiyostahimili ukame.

Zakaria amesema ili kukabiliana na tatizo hilo ni vyema serikali ikachimba visima ili shughuli za kilimo zisiwe za msimu na wajikite katika kilimo cha umwagiliaji.

“Visima vikijengwa tutaachana na kilimo cha kutegemea mvua na ninadhani hata tatizo la kuzagaa kwa ombaomba Dodoma litapungua,” amesema mkazi huyo.

Mkoa wa Dodoma upo tofauti na mikoa mingine ambayo inakabiliwa na njaa, huu kwa sura unaonekana ni kame lakini ukiutizama kwa kilimo si kame kwani una ujazo wa maji ya kutosha kuliko maeneo mengine ukichimba futi 12 yanapatikana maji ya kutosha.

error: Content is protected !!