Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakandarasi wanaichonganisha serikali na wananchi
Habari Mchanganyiko

Wakandarasi wanaichonganisha serikali na wananchi

Suleiman Jaffo, Naibu Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Spread the love

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) Suleiman Jafo amewaambia wakandarasi kutotimiza wajibu wao na kukamilisha kwa muda muafaka miradi wanayopewa na mamlaka za serikali ni kuwachonganisha kwa wananchi, anaandika Dany Tibason.

Mbali na kuwagombanisha na wananchi lakini kitendo cha kuingiza ubabaishaji katika utendaji wao wa kazi wanasababisha kuchelewesha maendeleo kwani miradi hiyo ikikamilika inachochea maendeleo.

Akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Wilunze wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma, Jafo amesema mkandarasi yeyote atakayepewa tenda ya mradi katika halmashauri yoyote nchini na asiitekeleze kwa wakati hataweza kupewa tenda mahali popote pale nchini.

“Kumekuwa na uzembe kwa wakandarasi nchini, mkandarasi anapewa kazi ya kujenga daraja, kujenga visima vya maji, barabara au mradi mwingine wowote katika halmashauri, badala ya kutekeleza mradi huo kwa wakati ili wananchi waendelee kupata huduma hiyo, yeye analeta uzembe na ubabaishaji, mtu wa namna hiyo hatutamvumilia katika serikali hii,” amesema Jafo.

Aidha, aliwataka wanakijiji wa Wilunze kuulinda mradi huo wa maji kwa kila mmoja kuwa msimamizi wa mradi na kuutaka uongozi wa kijiji kuhakikisha kuwa kinaundwa chombo cha watumiaji wa maji kijijini hapo ambacho kitakuwa na wajibu wa kusimamia mradi huo.

Mradi wa maji wa kijiji cha Wilunze uliozinduliwa leo ni mmoja kati ya miradi ya maji ya vijiji 10 inayojengwa wilayani Chamwino kupitia Programu ya Maji Vijijini. Mradi huo uliojengwa na Mkandarasi M/S Kijima Contractors akisimamiwa na Ofisi ya Mhandisi wa Maji Chamwino umegharimu jumla ya sh. 347,909,621.

Kwa upande wake Mbunge wa Chilonwa, Joel Mwaka amemshukuru naibu waziri na serikali kwa ujumla kwa kuwapatia huduma ya maji safi wananchi wake na kuwasisitiza wananchi kuuliunda mradi huo kwa hali na mali kwani umeigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha katika utekelezaji wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!