December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wakandarasi: Sekta binafsi inafanya vizuri kwenye ujenzi

Spread the love

MWENYEKITI wa Chama cha Wakandarasi wazawa nchini Tanzania, Mhandisi Thobias Kiando, amesema takwimu mbalimbali duniani zinaonesha kuwa sekta binafsi inafanya vizuri zaidi ya sekta ya umma kwenye kazi za ujenzi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Hivyo ameiomba Serikali licha ya kutaka kubana matumizi kwa kutumia zaidi sekta ya umma, iangalie zaidi ubora wa miundombinu na muda ambao miundombinu itadumu.

Kiando ameyasema hayo jijini Dodoma jana tarehe 4 Juni, 2022, wakati akisoma risala ya wakandarasi na wahandisi wazawa kwenye kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha wakandarasi wazawa.

“Tumeshuhudia sekta binasfi kufanya vizuri kuliko sekta ya umma katika ujenzi, usimamizi mzuri wa rasilimali fedha, rasilimali watu na vitendea kazi. Sekta binasfi iendelee kuaminiwa na kuwezeshwa kwa kupewa kazi,” amesema.

Amesema pamoja na Serikali kutaka kupunguza matumizi ya fedha ili zutumike kwa shughuli zingine tunaamini hili linahitaji fikra pana zaidi hasa kwa kuzingatia thamani ya fedha.

Amesema thamani ya fedha inaangalia pia muda ambao miundombinu itadumu na ni kwa kiasi gani itahitaji ukarabati baada ya kukamilika.

Kiando amesema katika kipindi kifupi cha uongozi wa awamu ya sita wameshuhudia ushirikishwaji mkubwa wa sekta binasfi katika ujenzi wa miundombinu tofauti na miaka ya nyuma.

“Katika muda mfupi wa Serikali ya Rais Samia tumeshughudia Serikali ikiongeza ushirikiano na sekta binafsi na tunaamini inatokana na imani yake binafsi kuwa sekta binafsi ndiyo injini ya kuleta maendeleo hivyo sekta ya umma lazima ishirikiane na sekta binafsi, amesema Kiando.

Amesema takwimu zinaonyesha kati ya miradi ya Sh 4.9 trilioni iliyosajiliwa mwaka 2021/22 miradi ya Sh 2.8 trilioni ilitolewa kwa wakandarasi wa ndani sawa na asilimia 57 tofauti na makandarasi wa nje Sh 2.1 trilioni sawa na asilimia 43.

Pia amesema wastani wa kusajili makampuni imekua kutoka wastani wa kampuni 850 hadi 900 miaka iliyopita na kufikia wastani wa kampuni 1,150 huku matarajio yakiwa ni kampuni 1300 kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa fedha.

“Haya ni mapinduzi makubwa maana miaka ya nyuma Makandarasi wa nje japo ni wachache walikuwa wakipewa kazi zenye thamani hata zaidi ya asilimia 70,” amesema Kiando.

Amesema wanatumani kwamba Serikali itaendelea kuwaamini wakandarasi wa ndani ili rasilimali za nchi zibaki h nchini kujenga nchi.

error: Content is protected !!