August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wajumbe wamtibua mwenyekiti wa CCM Katavi

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

Spread the love

MWENYEKITI wa CCM wa Mkoa wa Katavi anayemaliza muda wake mwaka huu, Mselemu Abdallah ameandika barua ya kujiondoa dakika za mwisho madai kuwa ametofautiana wajumbe wa halmashauri Kuu ya CCM mkoa huo, anaandika Mwandishi Wetu.

Akizungumza na wajumbe, Mselemu alikiri kuandika barua ya kujiondoa kugombea nafasi hiyo na tayari ameishakabidhi kwa Katibu wa CCM wa mkoa wa Katavi.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya kikao cha halmashauri kuu ya CCM, kilichofanyika wiki iliyopita katika ukumbi wa CCM wilaya ya Mpanda, kada huyo kajiondoa baada ya kutofauatina na wajumbe wa kikao.

Inadaiwa kuwa siku hiyo kikao hicho kilichokuwa kikiongozwa na yeye kilikuwa kinawajadili na kuwapitisha majina ya wana CCM waliokuwa wakiomba kuteuliwa kugombea nafasi mbalimbali.

Mwenyekiti huyo alikuwa hataki baadhi ya wagombea majina yao yapitishwe na kikao hicho wakiwemo baadhi ya viongozi wa sasa wanaotoka kwenye baadhi ya kata na wengine ambao yeye alikuwa amewasimisha uongozi.

error: Content is protected !!