JUMLA ya wanachama wa 1,862 Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho, wamehudhuria mkutano huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).
Rodrick Mpogolo, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara amesema, wajumbe waliotakiwa kuhudhuria mkutano huo leo tarehe 30 Aprili 2021, jijini Dodoma ni 1,876 ambapo idadi kamili ya wajumbe hao huwa 1,909 hivyo kufanya upungufu ya wajumbe 33.
Mpogolo amesema, idadi hiyo ya wajumbe kwa asilimua 99 imefanya akidi iliyohitajika kutimia na kufanya mkutano huo kuwa halali kwa mujibu wa Katiba ya CCM.
Rodrick Mpogolo, Kaimu katibu Mkuu (CCM)
Mpaka sasa, tayari kura za kumchagua mwenyekiti mpya wa chama hicho imefanyika. Kwenye nafasi hiyo, kuna mgombea mmoja – Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wa Tanzania. Kura zinahesabiwa.
Uchaguzi mwingine unaoendelea kwenye mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete ni wajumbe wawili wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, ili kujana nafasi mbili zlilo wazi.
Tayari kura zimepigwa ambapo wamejitokeza wajumbe sita ambao ni Nguvu Edward Chengula (Iringa), Ashrafu Sadru Kiyokya (Kagera), Kurwa Solo Majiyabululu (Tanga), Happyness Wiliam Mgongo (Dodoma), Fadhili Salum Mgenzi (Kigoma) na Reshma Othman (Kigoma).
Leave a comment