Sunday , 3 December 2023
Home Kitengo Maisha Afya Wajawazito wahimizwa kupima Ukimwi
Afya

Wajawazito wahimizwa kupima Ukimwi

Spread the love

AKINA Mama wajawazito wametakiwa kuwahi kliniki mara wanapohisi wana ujauzito na kufuata ushauri wa wataamu wa afya ili kuwakinga watoto wanaotarajia kujifungua dhidi ya maabukizi ya Virus vya UKIMWI. Anaripoti Khalifa Abdallah … (endelea).

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa huduma za kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Leonard Subi mjini Dodoma hivyo kuwataka wananchi kuchukua hatua katika kujikinga na maradhi mbalimbali ikiwemo Virusi Vya Ukimwa (VVU).

Amesema Utafiti uliofanywa mwaka 2010 maambukizi ya Virus yalikua asilimia 26 kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto huku utafiti uliofanywa mwaka 2016/2017 unaonesha kuwa maambukizi haya yamepungua na kufikia asilimia 7.6 ambapo Serikali imesema inatarajia maambukizi haya yapungue mpaka asilimia 2 ifikapo 2020-2021.

“Ni muhimu kwa wajawazito kuhudhuria kliniki na kupima VVU hii itasaidia kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, malezi na makuzi mzuri ya Mtoto yanategemea wazazi wote wawili yaani baba na mama wazazi wote wanaaswa kushirikiana hasa katika kupima afya afya ili mtoto atakaezaliwa asiwe na maambukizi ya VVU”Alisema Dkt.Subi.

Aliongeza kuwa moja ya changamoto inayokwamisha mpango huu ni wanaume kukumbatia mila na destuli za kutoandamana na wenzi wao kliniki wakati wa kipindi cha ujauzito,“hivyo familia au makabila ambayo bado yanaona kwamba mwanaume kumsindikiza mwenzi wake kliniki ni kujishushia hadhi waachane nazo.”

Aidha, Dkt.Subi amewataka vijana kuchukua hatua za kwenda katika vituo vya afya kupata elimu ya uzazi na kupima afya zao maana wao ndio mama au baba wanaotarajiwa,mimba za utotoni ni hatari kwa afya zao na kama kuna tatizo lolote wafike katika vituo vya afya ili kupata msaada wa kitalaamu.

Alisisitiza kuwa vituo vya kutolea huduma za afya vyote nchini hivi sasa vinatoa huduma ya elimu bure kuhusiana na afya ya uzazi na endapo mama mjamzito atagundulika ana maambukizi ya VVU ataanzishiwa dawa ambazo zitamkinga mtoto asizaliwe na maambukizi ya Virus vya UKIMWI.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Majaliwa aipongeza GGML mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveWaziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining...

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaMichezo

GGML yatoa milioni 17 kung’arisha ATF Marathon

Spread the loveKATIKA kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kukabiliana na maambukizi...

Afya

‘Ambulance’ yawarejeshea tabasamu wananchi Mkuyuni

Spread the loveWananachi wa  Tarafa ya Mkuyuni, Halmashauri ya Morogoro mkoani Morogoro,...

error: Content is protected !!