February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wajasiliamali wapigwa msasa kuzalisha bidhaa bora

Baadhi ya wajasiriamali wakiwa katika viwanja vya Nyamagana, Mwanza wakionesha bidhaa zao.

Spread the love

MENEJA Mkuu wa Kampuni ya Chef Asili Co.LTD mkoani Dodoma Lupyana Chengula, amesema kuwa ili wajasiriamali waweze kufanikiwa kwenye fursa zao za biashara wanatakiwa kutengeneza bidhaa zenye ubora na zinazoweza kuingia katika ushindani wa masoko ya ndani na nje, anaandika Dany Tibason.

Kwa kufanya hivyo watakuwa wanaunga mkono serikali juu kauli ya Rais John Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa na nchi yenye uchumi wa viwanda na biashara.

Chengula amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa kwa upande mwingine kwa kufanya hivyo watakuwa wanatimiza suala la kuwekeza kwenye viwanda hapa nchini.

Amesema wajasiriamali wanatakiwa kuwekeza viwanda vya kisasa ambavyo vitakidhi mahitaji ya soko litakalolingana na ushindani.

Aidha aliwataka wajasiriamali wa mkoa wa Dodoma kuhakikisha wanazalisha bidhaa zilizo bora kulingana na mahitaji na ushindani wa soko, ambapo kwa hivi sasa tumekuwa tukipokea wageni wengi.

Amesema katika uzalishaji huo wa bidhaa pia wazingatie viwango ambavyo vitakidhii vigezo na sifa toka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa matumizi ya mlaji.

“Ni muhimu wajasiriamali tukawa makini kwenye utegenezaji na uzalishaji wa bidhaa zetu, tukahakikisha zinakuwa nembo ambazo kwa kushirikiana na TBS pia wamedhihakiki kwa matumizi ya mlaji,” amesema.

Amesema kuwa kutokana na mpango mzuri wa serikali kusisitiza kuwepo kwa viwanda hapa nchini wajasiriamali lazima tujiadhali na viwanda ambavyo vitakuwa vikiharibu soko letu.

Aidha amewataka pia wajasiriamali hao kuhakikisha wanafanya shughuli zao ueledi na ubunifu, ili waendane na kasi iliyopo ambayo serikali imekuwa ikihimiza kuwepo kwa viwanda hapa nchini.

error: Content is protected !!