March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waitara: Wathubutu waone

Spread the love

NAIBU Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mwita Waitara amesisitiza kuwa, marufuku ya wazazi kuchangishwa michango ya wananfunzi shuleni ibaki pale pale na kwamba, walimu wasithubutu kukiuka agizo hilo. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Waitara ambaye ni Mbunge wa Ukonga, Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametamka hayo wakati wa ziara ya kushukuru wananchi wa jimbo lake waliopo kwenye Kata ya Chanika ikiwa ni baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge Ijumaa iliyopita.

Akiwa kwenye ziara hiyo jimboni kwake Waitara amesema, utaratibu wa kuwaandikisha watoto wote waliofika uamri wa kwenda shule katika elimu ya awali na msingi unapaswa kutekelezwa kwa kuwa ndio sheria inavyoelekeza.

Mbunge huyo ambaye awali alitokana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amewaeleza wakati wa Chanika kuwa, ataendelea na oparesheni ya kuhakikisha wanafunzi wanaandikishwa shule huku akiahidi kuwa, wataothubutu kukwamisha utekelezwaji wa agizo hilo kutokana na michango atakiona.

“Nasimamia kwa karibu suala la elimu, michango yenye kero imeondolewa, watoto darasa la awali, la kwanza na kidato cha kwanza waandikishwe, hii ni oparesheni ya kuhakikisha wanaandikishwa.

“Ni marufuku kuzuia mwanafunzi kujiunga darasa la awali, la kwanza na kidato cha kwanza kama mzazi wake hajatoa michango, ukizuiliwa kuandikisha mtoto sababu hujatoa mchango toa taarifa,” amesema Waitara.

Amesema Serikali inakataza michango yenye kero hivyo atakayezuia watoto kuandikishwa kwa sababu hiyo atachukuliwa hatua.

error: Content is protected !!