Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waitara alia tena, wabunge wamcheka… atoka bungeni
Habari za Siasa

Waitara alia tena, wabunge wamcheka… atoka bungeni

Spread the love

 

MBUNGE wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (CCM) leo Jumanne ameangua tena kilio bungeni na kutoka nje ya ukumbi wa mhimili huo kwa madai ya kutoridhidhishwa na majibu ya Serikali kuhusu malipo ya fidia katika maeneo ya Mgodi wa Barrick North Mara Komarera, Nyamichele na Murwambe. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Tukio hilo limejiri leo tarehe 9 Mei 2023 bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu Waitara alihoji ni lini wananchi hao watalipwa fidia.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Madini, Stephen Byabato amesema mgodi wa Barrick North Mara ulionesha nia ya kutaka kuchukua baadhi ya maeneo ya Vijiji vya Komarera, Nyamichele na Murwambie ambavyo ni sehemu ya Vijiji vinavyozunguka mgodi huo.

“Baada ya Wananchi wa Vijiji hivyo kupata taarifa ya maeneo yao kuhitajiwa na mgodi wa Barrick North Mara, walianza kuongeza majengo harakaharaka (maarufu kama Tegesha), hali hiyo ilipelekea mgodi huo kuachana na maeneo hayo kwani hayaathiri uendeshaji wa shughuli zao za kila siku,” amesema.

Baada ya majibu hayo, Waitara badala ya kuuliza swali la nyongeza kama ulivyo utaratibu wa Bunge, alisimama na kuanza kulalamika kutoridhishwa na majibu na kutoka nje ya Bunge baada ya kuzozana kwa muda.

Licha ya kutakiwa kuuliza swali la nyongeza, Waitara aliendelea kung’aka huku akitoa sauti ya kilio jambo ambalo baadhi ya wabunge walimcheka huku wengine wakimwambia pole.

Hata hivyo, Waitara ambaye mwaka 2015-2020 alikuwa ambaye alikuwa mbunge wa Ukonga kabla ya kutimkia Tarime vijijini, alianza kuvua tai na koti lake wakati akitoka nje ya Bunge na kusema wanatarime leo wamemjua mbaya wao.

Hii ni mara ya pili Waitara kumwaga machozi kwani tarehe 28 Machi mwaka huu, aliangua kilio mbele ya waandishi wa habari baada ya kutokea mgogoro kati yake na uongozi wa Mkoa wa Mara hali iliyopelekea Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Janerali Suleiman Mzee kumtaka asikwamishe zoezi la uwekaji wa bikoni mpakani mwa eneo eneo la hifadhi na makazi ya wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

error: Content is protected !!