May 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waislam wamporomoshea dua JPM

Rais John Magufuli

Spread the love

SWALA ya Eid Alhaj iliyoswaliwa kitaifa jijini Dar es Salaam imemalizika kwa kuombewa dua Rais John Magufuli. Anaripoti Yusuph Katimba … (endelea).

Dua hiyo imeendeshwa na Kaimu Mufti, Khatib Jongo mbele ya Waumini wa dini hiyo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya mgeni rasmi Hussein Alli Mwinyi ambaye ni Waziri wa Ulinzi kufikisha Salam za Eid kutoka kwa Rais Magufuli.

Katika Salam hizo Rais Magufuli aliwaomba masheikh kumwombea dua ili aweze kuongoza kwa amani.

Kauli baada ya maombi hayo, Sheikh Jongo alisimama na kuendesha dua hiyo fupi na kuitikiwa na waumini waliohudhura swala hiyo.

Kwenye Salam zake kwa Waislam, Waziri Mwinyi amesema kuwa, Waislam Ni sehemu muhimu kwa Waislam hivyo jukumu la amani ni muhimu kulitekeleza.

Ameeleza kufurahishwa na uongozi wa Mufti wa Tanzania, Abubakar Zuberi kutokana na kubadili taswira ya baraza hilo.

Amesem kuwa, uamuzi wa Bakwata kujitathmin miongoni mwa mambo muhimu kwenye taasisi hiyo.

Pamoja na mambo mengine Bakwata imepanga kuanzisha viwanda ili kutoa ajira kwa vijana.

Kauli mbiu ya Bakwata chini ya Mufti Zuberi ni Jitambue, Badilika, Acha Mazoea.

error: Content is protected !!