June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waislam wagawanyika vipande vipande

Spread the love

WAUMINI wa dini ya kiislamu nchini wmegawanyika katika makundi mawili ya siasa ambapo upande mmoja wanaunga wa Umoja wa Katiba ya Wananchi na upande mwengine wanasapoti Chama cha Mapinduzi CCM. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Wakizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam,Kamati ya Mashekh na Maimamu Jijini Dar es Salaam kupitia Mwenyekiti wa kamati hiyo Shekh Said Rico, amesema kuwa Baraza la Waislamu Mkoani Mwanza wameshindwa kuzungumzia matatizo ya waislam badala yake kumshambulia Mgombea Urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Edward Lowassa.

Amesema rafiki wa Mgombea huyo na Askfu Gwajima kuwa sio kigezo cha kusema mgombea huyo ana udini kutokana na kuwa mgombea huyo alialikwa na mashekh hao katika uchangiaji wa Radio ya kiislamu ya Iqra Fm ambapo alichangia mchango mkubwa ambapo mashekh hao walimvisha Joho na kilemba na Kumpa jina la Abdallah.

“tunawaomba waislam wapuuze mashekh hawa wa Mwanza sisi tunaweka msimamo wetu wazi kuwa tunataka mabadiliko kutokana na kuchoshwa na mateso na manyanyaso wanayoyapata Mashekh wetu, ambao wapo magerezani na wakilalamika kuwa wanafanyiwa matendo mabaya na kwamba hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ilhali madrasa wamesingiziwa kesi za Ugadi na kufunga baadhi ya madrasa”amesema Rico.

Amemesema kuwa waislam wanasikitishwa na kitendo cha shekh Ponda kuendelea kuwekwa gerezani kwa kipindi cha miaka miwili na miezi mitatu bila ya kupewa dhamana ambapo kesi yake inapaswa kuwepewa dhamana kisheria

“Sisi waislamu tunaenda kutoa hukumu yetu siku ya juma pili Oktoba 25 hatuma haja ya maandamano wala hatufanyi fujo bali tutatumia vizuru fursa hiyo ya kupiga kura kwa kupata kiongozi takayeweza kutenda haki kwa waislam na wananchi wote’’ amesema Rico.

Katika kuadhimisha sherehe za Mwaka Mpya wa Kiislam 1437 (02.01.1437, Baraza la Waislam Mkoa wa Mwanza kupitia kwa Katibu Mkuu, Mkoa Mwanza Sheikh Mohamed Balla alitoa tamko kutokana na kauli inayoelezwa kutolewa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kwamba ana ndoto ya Misikiti yote nchini kugezwa kuwa Sunday School na Masheikh watakwenda kuangukia katika misalaba.

Alisema kauli za namna hiyo si njema kwa mstakabali wa Taifa ambapo alisema kuwa waislamu wote Mkoani Mwanza wanalaani na kukemea kauli hiyo na nyingine zote za aina hiyo na wale wanaozitoa.

Aliwataka Watanzania kuungana kwa pamoja hususani katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu na kwamba Wamchague kiongozi muadilifu, Mchapakazi na anaechukia rushwa ambae ataendelea kuwaunganisha watanania wote.

error: Content is protected !!