Saturday , 13 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Waislam Dodoma wapewa somo
Habari Mchanganyiko

Waislam Dodoma wapewa somo

Waumini wa kiislam mkoani Dodoma wakiwa katika swala
Spread the love

WAUMINI wa Dini ya Kiislamu Mkoa wa Dodoma wametakiwa kuzikamata fursa kutokana na Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi, anaandika Dany Tibason.

Mbali na waumini wa dini hiyo kutakiwa kukamata fursa ya kuishika makao makuu pia wametakiwa kuchapa kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni na kuendekeza fitina na uchonganishi.

Rai hiyo imetolewa jana na Mustafa Rajabu, Sheikh wa Mkoa wa Dodoma alipotoa nasaha zake kwa waumini wa dini hiyo katika Msikiti wa Mtoro Maili mbili darajani mjini hapa.

Sheikh Rajabu akitoa nasaha hizo katika ibada ya Maulidi msikitini hapo amesema, ni vyema sasa waumini wa dini hiyo kuchapa kazi kwa maslahi yao wenyewe na jamii kwa ujumla.

Amesema kama waumini wa dini hiyo hawatakuwa na tabia ya kusoma alama za nyakati katika kuzishika fursa zinazopatikana ni wazi kuwa, waumini hao watabaki kuwa nyuma.

Katika hatua nyingine amesema, waumini wa dini ya kiislamu wanatakiwa kuwa watu wa tabia njema kwa kupendana na kuondokana na fitina pia kupikiana majungu jambo ambalo ni kinyume na mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Muhammad (S.A.W).

Mbali na hilo, amewataka wazazi ambao ni waumini wa dini ya kiislamu kuhamikisha wanapeleka watoto shule pia wakitenda muda wa madarasa.

Hussein Hasani, Sheikh katika Msikiti wa Chang’ombe mjini humo amesema, kitendo cha kururejeshwa shehe wa mkoa katika nafasi hiyo ni kuufanya Uislam usawi katika mkoa huo.

Mbali na hilo amesema kuna kila sababu ya kumwombea sheikh huyo wa mkoa ili kumuepusha na misukosuko ya kiuongozi.

“Yapo mashetani na majini ambayo ambayo uweza kumwandama lakini pia anatakiwa kumtia nguvu na kumwondolea uoga wa kuuongoza Mkoa wa Dodoma. Tunajua kazi hii ni vita hivyo kijana wetu tumuombee,’ amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askofu ataka mafisadi, wauza mihadarati washughulikiwe kumuenzi Sokoine

Spread the love  MHASHAMU Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Isaac...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mafuriko yaua 33 Morogoro, Pwani

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetoa tathmini ya athari ya mafuriko...

Habari Mchanganyiko

Wanafunzi 7 wahofiwa kufariki gari la shule likitumbukia korongoni

Spread the love  WANAFUNZI saba wanahofiwa kupoteza maisha, huku watatu wakinusurika katika...

Habari Mchanganyiko

Wazazi, walezi watakiwa kuwa karibu na watoto wao

Spread the love  WAZAZI na walezi wameagizwa kuwalea watoto wao katika maadili...

error: Content is protected !!