August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waichongea CRDB kwa Rais Magufuli

Spread the love

WANACHAMA wa kikundi cha wakulima wa tumbaku (Tumaini Itave Association) cha Urambo, Tabora  wamemtaka Rais John Magufuli kuingilia kati mgogoro uliopo kati yao na benki ya CRDB, Anaandika Aisha Amran.

Kauli hiyo imetolewa na Moshi Lubibi, mwakilishi kutoka katika kikundi hicho, alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Amesema mwaka 2014/15 kikundi hicho kiliingia makubaliano ya kuuza tumbaku yake kupitia chama cha ushirika cha Itundu Amcos, baada ya kikundi hicho kushindwa kukidhi matakwa ya usajili wa Bodi ya Tumbaku ya Taifa.

Amesema  katika makubaliano hayo, Amcos walikubali  kikundi hicho kiuze tumbaku kupitia kwenye ushirika wao hivyo na Tumaini Itave, iliomba kuuza kilo 70,000 kwa kampuni ya TLTC kwa gharama ya Dola za Kimarekani  98,770.216 ambapo malipo yake yalipaswa kufanyika kupitia benki ya CRDB tawi la Urambo.

“Kabla ya malipo hayo, kufanyika kikundi hicho kiliwajulisha CRDB kuwa malipo yao yanapitishiwa katika Akaunti ya Itundu  Amcos, ambao ni wateja wao, lakini mara baada tu ya TLTC kufanya malipo mmoja wa maofisa wa benki hiyo, alitutaka tumpe rushwa ya dola za kimarekani 10,983 ndipo akamilishe malipo yetu,” Amesema  Lubibi.

Amesema Septemba, 2015, walipeleka malalamiko yao kwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo na kufuatilia bila mrejesho na kwamba hali hiyo ilisababisha wachukue uamuzi wa kuwasiliana na Margreth Sitta, Mbunge wa Urambo Mashariki.

“Mama Sitta alituunganisha na Dk. Florence Turuka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ambapo naye alituomba tumpe nafasi ili awasiliane na watu wa CRDB ili kujua undani wa jambo lenyewe.

Dk. Florence alimuagiza Mkurungezi wa Bodi ya Tumbaku kufanya uhakiki, ambapo baada ya uhakiki kufanyika ilibainika kuwa TUMAINI ITAVE iliuza Tumbaku kilo 51,741 ambayo iliuzwa kupitia Itundu AMCOS na kumtaka Mkurungezi mkuu wa CRDB kuwalipa wakulima hao haki zao stahiki.” Amesema.

Lubibi amedai kuwa, ni wakati muafaka sasa wa Rais Magufuli kuingilia kati suala hilo kwani pamoja na jitihada hizo, CRDB iligoma nab ado imegoma kulipa fedha hizo mpaka sasa.

 

error: Content is protected !!