April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wahudumu wodi ya corona Kenya wagoma

Spread the love

MGOMO umeibuka katika wodi iliyotengwa kuwahudumia watu walioambukizwa virusi vya corona nchini Kenya. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Taarifa zaidi kutoka nchini humo zinaeleza, wahudumu wa wodi hiyo wamelalamika kutokuwa na vifaa kamili vya kujikunga, ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mafunzo ya kutosha.

Hospitali ya Mbagathi katika mji mkuu wa Nairobi, ni moja ya hospitali zilizo na wodi ya kutibu wagonjwa waliombukizwa virusi hivyo hatari.

Hospitali hiyo ina juma ya watu 22 waliokuwa karibu na mtu wa kwanza aliyebainika kuwa na virusi vya corona kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Seth Panyako, Katibu Mkuu wa Muungano wa Wauguzi Kenya amesema, wauguzi watarejea kazini kama serikali itawapa mavazi maalum na mafunzo ya jinsi ya kuwashughulikia wagonjwa hao.

Cyrus Oguna, msemaji wa serikali ya Kenya amekiri kuwepo kwa upungufu na changamoto kadhaa, hata hivyo amesema, serikali itatoa maelezo zaidi shughuli hiyo imefika wapi.

error: Content is protected !!