Thursday , 2 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Wahitimu watakiwa kuwa waadilifu
Habari Mchanganyiko

Wahitimu watakiwa kuwa waadilifu

Amir wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Tahir Chaudry (aliyekaa) akifungua maktaba mpya katika chuo cha Jamia Ahmadiyya Morogoro.
Spread the love

 

WAHITIMU wa elimu ya dini wa Chuo cha Jamiah Ahmadiyya kilichopo Kihonda Maghorofani katika manispaa ya Morogoro wametakiwa kuwa waadilifu na mfano mzuri kwa jamii pindi wanapoenda kutekeleza majukumu yao ya kufundisha. Anaripoti Ashura Kazinja, Morogoro … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo tarehe 6 Disemba, 222 na Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania, Sheikh Tahir Mahmoud Chaudry kwenye mahafali ya 38 ya kuwaaga wahitimu wanaomaliza masomo yao chuoni hapo.

Alisema kuwa ili waweze kuheshimiwa na kuthaminiwa katika jamii ni vyema wakawa mfano mzuri kwa kutenda yaliyo mema.

Sheikh Chaudry  aliwasisitizia wahitimu hao kujiendeleza zaidi kielimu hasa kwa kusoma vitabu mbalimbali vitakavyowasaidia kupata uelewa na ujuzi katika elimu hiyo ya dini ya Kiislam.

“Jambo la muhimu sana ni vitendo, kama tumemuamini Mtume Muhammad na Quruan basi tufate matendo yake, kwa kuwa sisi ni walimu hivyo ni vyema kufuata matendo yote mema kama ishara ya kumtii Mungu” alisema Sheikh Chaudry.

“Mwenendo wetu ni muhimu sana jinsi tunavyoishi au kukaa na watu, tukitoka nje muonekano wetu na mavazi yetu yakoje, tabia zetu na hata namna ya kuongea tunatizamwa na watu tunaongea nini na kwa namna gani” aliiongeza

Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Sheikh Mahmoud Bhatti alisema kuanzia mwakani wanatarajia kuboresha zaidi mazingira pamoja na mitaala ya kufundishia ili waweze kutoa elimu bora zaidi.

“Miaka hii miwili tutaitumia kuboresha mitaala na kuangalia vitu gani havipo ili viongezwe kwenye silabasi, mwakani tunapoanza tunaanza mtaala mpya, Mungu atatusaidia kufikisha malengo yetu ya kuboresha elimu” alisema Sheikh Bhatti.

Akitoa ripoti ya chuo kwa mwaka 2022 Mwalimu Shamuni Juma alisema kuwa pamoja na masomo ya darasani pia chuo kimeweka utaratibu wa program maalum ambayo lengo lake ni kuwajenga na kudumisha nidhamu za wanafunzi hao.

Mwalimu Shamuni aliongeza kuwa hadi sasa chuo kimefanikiwa kuwapeleka wanafunzi 20 nchini Ghana ambao wameenda kujifunza zaidi elimu ya dini , wakiwemo wanafunzi wengine watatu walioenda mwaka huu.

Hata hivyo mahafali hayo ya 38 yameenda sambamba na ufunguzi wa maktaba mpya yenye vitabu mbalimbali ikiwemo Quruan na Kompyuta, ambayo ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 29.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

GGML kuwapatia mafunzo kazi wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini

Spread the loveJUMLA ya wahitimu 50 wa vyuo vikuu nchini wamepata fursa...

Habari Mchanganyiko

NHC yaongeza mapato kufikia kufikia Sh bilioni 257

Spread the loveSHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeongeza mapato hadi kufikia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mo Dewji achomoza bilionea pekee Afrika Mashariki

Spread the loveMAZINGIRA mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania yamezidi kuleta matunda baada...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia: Panapotokea uvunjifu wa amani panakuwa haki imepotezwa

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu...

error: Content is protected !!