Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Wahitimu wa kidato cha sita watakiwa kuwa ndoto na mipango madhubuti
Elimu

Wahitimu wa kidato cha sita watakiwa kuwa ndoto na mipango madhubuti

Spread the love

KAMISHNA wa Utawala na Raslimali watu wa Jeshi la Polisi nchini, C.P Suzan Kaganda amewataka vijana  hasa wasichana ambao ni wahitimu wa kidato cha sita kuwa na ndoto kubwa na mipango madhubuti ya kuweza kuzitimza ndoto hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

C.P Kaganda aliyasema hayo jana wakati wa mahafali ya 17 ya kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Barbro Johansson kampasi ya Luguruni jijini Dar es Salaam.

Kaganda alisema ni muhimu kwa wasichana nchini kuwa na ndoto kubwa ambazo zinapimika na zinaweza kutekelezeka kwa wakati na muda sahihi huku wakizingatia maadili na kuwa chachu ya mabadiliko yaliyomema yenye kuzingatia utu na usawa.

“Kuweni na ndoto ambazo matokeo yake yanapimika na kutekelezeka, daima nawaombea kwa Mungu ili muweze kuwa na mafanikio makubwa ya kuweza kuzifikia ndoto zenu, kwa kuzingatia upendo na mshikamano iIi kuweza kuyabadili yale magumu kuwa mepesi.

“Mkumbute tu ukitaka kufika haraka nenda peke yako ila ukitaka kufika mbali nendeni kama team yaani pamoja, mkiwa na upendo na mshikamano wa kweli itawasaidia kufika mbali zaidi kwa pamoja na kupata mafanikio,” alisema Kaganda.

Aidha aliwataka wasichana hao kuwa makini na utadawazi kwani unaweza kuwa na athari katika malezi na ukuaji wao na kwamba wanapaswa pia kuwa wakweli wa nafsi zao kwa kusimamia mambo wanayoyaamini maishani bila kuvunja sheria za nchi, shule na za nyumbani ambazo wazazi wameziweka.

“Kutokana na utandawazi wapo wengine utawaheshimu lakini wanaweza kukuvunjia heshima yako hivyo wasichana mnapaswa kuwa makini na wadadisi wa mambo na muwe na kiasi katika kupima na kutoa heshima hiyo, msitoe heshima kwa mtu ambaye hawaheshimu ili msije kuingia katika mitengo ya kidunia,” alisema

Aidha alisema vijana wanapaswa kutambua kuwa elimu haina mwisho hivyo wasiache kujifunza na kuchukue ujuzi, maadili, mila, desturi,  uvumilivu na uthubuti waliojifunza kutumia katika kuleta mabadiliko chanja kwenye jamii.

Kuhusu chagamoto inayoikabili shule hiyo ya upatikanaji wa fedha za kufadhili wasichana ambao familia zao zinakipato kidogo, alisema amewataka watu wenye uchungu na elimu kujitokeza katika kuwachagia wanafunzi wenye sifa kupata elimu katika shule hiyo.

“Jukumu la kusaidia elimu ni letu sote kama jamii, sisi tutaangalia litakalowezekana ili kuweza kusaidia ila tunawaomba watu wengine kujitokeza kusaidia kundi hili, pia nafahamu juu ya changamoto ya  ardhi ya shule kuvamiwa na waarifu, niwaombe viongozi wa serikali mliopo hapa kuitafutia suluhisho la kudumu jambo hili,” alisema

Aidha Kaganda aliishukuru Serikali na marafiki wa Sweden ambao wameendelea kutoa msaada katika shule hiyo kwa kuwasomesha wasichana wenye mahitaji maalum katika shule hiyo.

Naye Mwenyekiti na Mwanzilishi wa shule hiyo, Profesa Anna Tibaijuka alisema anaishukuru Wizara ya Elimu kwa kuachana na masuala ya kupanga shule 10 bora katika matokeo ya mitihani ya kitaifa na badala yake kuzipatia daraja shule kwa namna zilizofaulisha wanafunzi.

“Ukisema huyu ni wa kwaza unapima nini, hali hii ilizifaya hule nyingi katika masuala ya kuiba mitihani ili waingie katika 10 bora, tunashukuru serikali kuliona hili na kuliondoa, sisi Barbro Johansson tunawajenga wasichana kufaya vizuri wakati wote na kujiamini ndio maana haturuhusu wanafunzi kuchapwa kiboko,” alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo, Jospina Leonidace alisema jumla ya wanafunzi 83 wanahitimu elimu ya kidato cha sita na kwamba wote wanandoto kubwa ya kujiendeleza zaidi kielimu ili waweze kulitumikia taifa.

Alisema wanafunzi hao wamelelewa ili waje kuwa viongozi bora wenye kuzingatia maadili na kufanya kazi kwa bidii kwani hiyo ndiyo silaha pekee kwao itakayowawezesha kufikia kilele cha mafanikio.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari

Serikali yataka vijana  wajiunge na program atamizi ya biashara CBE

Spread the love  SERIKALI imewahamasisha vijana kujiunga na program atamizi inayotolewa na...

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na...

Elimu

Harambee ujenzi sekondari za Musoma Vijijini yashika kasi

Spread the love  HARAMBEE ya ujenzi na ukarabati wa shule za sekondari...

error: Content is protected !!