Monday , 27 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu ‘Wahitimu Kidato cha IV wachangamkie fursa hii’
Elimu

‘Wahitimu Kidato cha IV wachangamkie fursa hii’

Wanafunzi
Spread the love

WANAFUNZI waliomaliza Kidao cha IV mwaka 2018 na matokeo yao kutangazwa, sasa wanaweza kutumia mfumo maalumu kubadili chaguo za masomo na tahasusi kulingana na ufaulu wa mitihani yao, kabla ya kupangiwa shule ama vyuo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Serikali imetoa fursa hiyo ili kuongeza wingi kwa mwanafunzi kusoma fani au tahasusi itakayomuandaa kuwa na utaalamu fulani katika maisha yake.

Seleman Jafo, Waziri wa Nchi,  Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kusudiuo la serikali kutoa fursa hiyo ya kufanya mabadiliko ya machaguo kwa utaratibu wa kujaza fomu inayoitwa ‘F4 Selform.’

Jafo amesema, fursa hiyo itawawezesha wanafunzi kurekebisha machaguo yao kulingana na ufahulu waliopata kwenye matokeo ya kidato yao yaliyopita hasa baada ya kujua masomo waliyofaulu vizuri.

“Hii ni kutokana na ukweli kwamba, baadhi ya wanafunzi hawakujaza kwa uhakika tahasusi au kozi zao kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufaulu katika masomo yao.

“Serikali kupitia TAMISEMI, imekamilisha zoezi la awali la kuingiza taarifa zilizo kwenye Selform za wanafunzi kwenye kanzi data ya TAMISEMI kama zilivyojazwa wakiwa shuleni kabla ya kuhitimu,” amesema Jafo.

Amesema, kwa sasa wanafunzi wataweza kufanya mabadiliko hayo kwa njia ya mtandao kadri watakavyonuia au kushauriwa. Na baada ya wanafunzi kufanya marekebisho hayo, kanzi data hiyo ndiyo itakayotumika kuwachagua na kuwapangia kidato cha tano na kozi za vyuo.

“Ili mwanafunzi aweze kuingia kwenye mfumo huu, itabidi kutumia namba ya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Nne, mwaka 2018, jina lake la mwisho, mwaka wa kuzaliwa na alama ya ufaulu aliyopata kwenye somo atakaloulizwa na mfumo au swali lolote atakaloulizwa.

“Ni matumaini yangu, watahitimu watatumia kwa ukamilifu fursa waliyopewa ya kubadilisha tahasusi na kozi kulingana na ufaulu walioupata ili waweze kusoma kozi au tahasusi ambazo wamefaulu vizuri,” alisema Jafo.

Amesema, zoezi hilo la kubadili tahasusi litafanyika kuanzia tarehe 1-15 Aprili 2019. Kutokana na muda huo uliopangwa kwa yeyote ambaye hatabadili taarifa zake TAMISEMI, itaamini kwamba ameridhika na machaguo yake ya tahasusi aliyofanya awali alipokuwa shuleni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

BiasharaElimu

Benki ya Exim yazindua huduma ya ‘Exim Smart Shule’

Spread the love  KATIKA juhudi za kuboresha teknolojia za kidijitali katika sekta...

Elimu

Waziri SMZ akoshwa na kazi za Global Education Link

Spread the loveSERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar SMZ imesema itaendesha msako na kuzifutia...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

error: Content is protected !!